27 August 2012

Miss East Afrika sasa kufanyika Des. 7


Na Neema Kalaliche

MASHINDANO ya Miss East Afrika kwa mwaka huu, yamepangwa kufanyika Desemba 7 badala ya Septemba katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam na yanatarajiwa kurushwa 'live' kupitia M-Net.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mtayarishaji Mkuu wa mashindano hayo, Lino Callist alisema wanatarajia zaidi ya watu milioni 200 duniani kuangalia mashindano hayo kwa njia hiyo.

Alisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba awali yalipangwa kufanyika Septemba lakini sasa yatafanyika Desemba na wamefanya hivyo ili kutoa zaidi kwa nchi ambazo hazijapata wawakilishi kukamilisha jambo hilo.

"Mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake ambapo yatashirikisha warembo kutoka katika nchi 16 za Ukanda wa afrika mashariki, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Alisema nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Pia nchi za Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Sudan Kusini, Malawi, pamoja na visiwa vya Shelisheli, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius zikishiriki kama nchi mwalikwa.

Alisema mashindano hayo yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania.

Nchi zilizopata wawakilishi wake mpaka sasa ni  Eritrea, Ethiopia, Uganda, Sudan Kusini, Malawi na Shelisheli.

No comments:

Post a Comment