24 August 2012

Kalala Junior arudi Twanga Pepeta



Na Zahoro Mlanzi

MSANII nyota wa muziki wa dansi nchini, Kalala Hamza 'Kalala Junior', amerejea katika bendi yake ya zamani, African Stars 'Twanga Pepeta'.

Msanii huyo ameamua kurudi rasmi katika bendi hiyo, baada ya kuondoka kwa miaka kadhaa ambapo alijiunga na bendi ya Mapacha Watatu.


Akizungumza Dar es Salaam jana Kalala Junior, alisema ameamua kurudi katika bendi hiyo baada ya kufanikisha kile kilichomfanya aondoke awali.

Alisema katika sanaa hasa ya muziki, imekuwa ni suala la kawaida kuhama bendi moja kwenda nyingine kwa ajili ya maslahi.

Mwanamuziki huyo alisema, Twanga Pepeta ni bendi kongwe nchini ambayo imemfanya afike alipo sasa hivyo ameamua kurudi, ili kuendeleza gurudumu la 'Amsha Amsha' ya Twanga Pepeta.

Alisema baada ya kurudi katika bendi hiyo mapema wiki hii, ameshakamilisha vibao viwili ambavyo anatarajia kuwitambulisha wakati wowote kuanzia sasa.

“Nimeamua kurudi katika bendi yangu ya zamani kwa ajili ya kuongeza nguvu baada ya kuondoka kwa muda, kuna kitu nilikuwa nakitafuta na nimeshakipata hivyo nimeamua kurudi nyumbani,” alisema.

No comments:

Post a Comment