16 August 2012
Dkt. Slaa afukuzwa nyumba ya wageni
Na Goodluck Hongo, Mikumi
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, juzi alifukuzwa katika nyumba ya kulala wageni iliyopo katika majengo ya Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), kilichopo Mikumi, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Dkt. Slaa aliwasili katika mji huo saa nane mchana akitokea tarafa ya Malinyi, wilayani Ulanga, akiwa katika operesheni iliyobeba jina la Vuguvugu la Mabadiliko.
Baada ya kufika katika nyumba hiyo, Dkt. Slaa alikabidhiwa funguo ya chumba alichoandaliwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Ulinzi wa chama hicho Bw. Alfred Lwakatare na kuingia chumbani.
Akiwa ndani ya chumba chake, alitokea Meneja wa Hoteli hiyo na kumweleza Dkt. Slaa kuwa chumba hicho kilishalipiwa na mteja mwingine hivyo alitakiwa kuondoka na kukabidhi funguo kwani hakukuwa na taarifa zozote za ujio wake.
Akizungumzia hali hiyo, Dkt. Slaa aliitupia lawama Serikali akidai ndiyo imehusika kuondolewa kwake katika nyumba hiyo ili kuzoofisha kampeni ya kuwakomboa Watanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment