16 August 2012

CHADEMA waibua ufisadi wa bil. 1.9/-



Na Goodluck Hongo, Kilosa

ZAIDI ya sh. bilioni 1.9, ambazo ni ruzuku zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ajiri ya miradi ya maendeleo zinadaiwa kutafunwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa,  aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Mnadani, vilivyopo Mji Mdogo wa Mikumi, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.


Alisema katika mradi wa UKIMWI, zaidi ya sh. bilioni nne zimepotea katika mazingira tata na hazijulikani zilipo.

“Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alihoji pesa hizi ziko wapi lakini hadi sasa hakuna majibu yaliyotolewa, halmashauri hii ilipewa fedha na Serikali zaidi ya sh. bilioni tatu kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya waananchi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Dkt. Slaa amemtaka Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, kuthibitisha madai yake kuwa CHADEMA kimepata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili wa nje lakini bado kinawahadaa Watanzania kwa kuwachangisha.

Alisema kama Bw. Nnauye atashindwa kuthibitisha madai hayo, chama hicho kitamtangaza katika mikutano yake kuwa ni muongo na mzushi.


No comments:

Post a Comment