16 August 2012

JWTZ leo kupiga mizinga 21 bandarini Dar



Na Mwandishi Wetu

MELI tatu za kivita kutoka Jeshi la Wanamaji nchini Japan, leo zitawasili Bandari ya Dar es Salaam, saa tatu asubuhi ili kufanya ziara ya kimafunzo kwa Maofisa wanafunzi waliomaliza mafunzo katika Chuo cha Japan Maritine Self Defence Forces (JMSDF).


Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), inasema meli hizo zitaongozwa na Rear Admiral Hidetoshi Funchinoue, ambaye ni Kamanda wa Mafunzo wa Vikosi vya Wanamaji na zitakuwa na mabaharia 1,176.

Alisema baada ya meli hizo kuwasili, itapigwa mizinga 21 ambapo kiongozi huyo atapata fursa ya kuzungumza na waandishi wa Habari.

“Sherehe za mapokezi ya meli hizo zitahudhuriwa na Balozi wa Japan nchini na Makamanda wa JWTZ, pia ujumbe huu utatembelea Bandari ya Dar es Salaam, Ofisi ya Meya wa Jiji na Makao Makuu ya Kikosi cha Navy Kigamboni,” imesema taarifa hiyo.

Kutokana na hali hiyo, JWTZ limesema mizinga hiyo ni baridi  na haina madhara yoyote kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment