16 August 2012
Alliance Academy waibuka mabingwa
Na Daud Magesa, Mwanza
TIMU za soka za shule ya vipaji maalumu ya Alliance School Sport Academy ya Mwanza, imeendelea kung’ara katika medani ya soka, baada ya kuibuka mwabingwa wa Kombe la Future Rafiki iliyofanyika jijini Arusha.
Alliance Academy inaundwa na timu za vijana wenye umri chini ya miaka 14 na 17.
Katika michuano hiyo, kikosi cha U-14 kilicheza mechi tatu na kujikusanyia pointi saba na mabao matano ya kufunga, baada ya kushinda michezo miwili na kutoka suluhu mmoja.
Kikosi cha U-17 kilizishinda tmu za Future Stars Academy bao 1-0, kabla ya kuibamiza Mamba Academy mabao 2-0 na kuhitimisha kwa kuipa kipigo cha bao 1-0 Young Life Academy na kufikisha pointi tisa na mabao manne.
Mashindano hayo ya Future Rafiki mbali na Alliance School Sport Academy iliyopeleka timu mbili za umri tofauti, ilishirikisha timu 8 za Arusha, ambazo ni Future Stars Academy, Habari Maalumu, Young Life na Mamba Academy.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili jijini hapa juzi ikitokea Arusha, kocha wa timu hiyo, Fulgence Novatus alisema michuano hiyo ilikuwa migumu kutokana na wapinzani wao kuwa na uzoefu.
Alisema pamoja na kuibuka washindi wa mashindano hayo ya Urafiki, iliwalazimu wachezaji wake kubadili mfumo na mbinu za uchezaji ili kupata ushindi na kufanikiwa kuwa vinara.
“Michuano ilikuwa migumu na yenye ushindani. Tulipata upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wetu ikizingatiwa wao wametangulia kuwekeza katika soka la vijana.
"Sisi tuna mwaka mmoja, lakini vijana wamejitahidi na wameonesha wako sawasawa wanazingatia mafunzo na maelekezo ya walimu,” alisema Novatus
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment