16 August 2012
Ajali yaua wawili, 42 wajeruhiwa
Na Patrick Mabula, Kahama
WATU wawili wamefaki dunia na wengine 42 kujeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea mjini Kahama, mkoani Shinyanga.
Basi hilo lilipunduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki ya abiria 'bodaboda', wakati likitokea mjini hapa kwenda Dar es Salaam, katika eneo la Nyasubu.
Ajali hiyo imetokea jana alfajiri ikihusisha basi lenye namba za usajili T 391 BWP, aina ya Scania linaloitwa “Leina Tours”, linalofanya safari zake kati ya Kahama na Dar es Salaam.
Mmoja wa majeruhi Bw. Kayumba Yusufu (52), mkazi wa Dar es Salaam, alisema basi hilo liliaguka mda mfupi baada ya kutoka Stendi Kuu ya Mabasi mjini Kahama, eneo Nyasubi jirani na Benki za Azania na NBC.
Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt. Andrew Emmanuel, alisema abiria mmoja aliyemtaka kwa jina la Happy John, mweye umri kati ya miaka 37-40, mkazi wa Tarime, mkoani Mara, alifariki hapo hapo.
Alisema dereva wa pikipiki Willison Paschal (24), ambaye inadaiwa ndiye aliyesababisha ajali hiyo, naye alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali kwa matibabu.
Dkt. Emmanuel alisema majeruhi waliofikishwa hospitari walikuwa 42, kati yao 27 waliumia vibaya na kulazwa wakiwemo wanaume 15, wanawake 12 ambapo 15 walipatiwa matibabu na kuruhusiwa.
Mkuu wa Polisi wilayani hapa, Bw. George Simba, alisema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Amini Amri, mkazi wa Dar es Salaam ambaye baada ya ajari alikimbia kusikojulikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment