02 July 2012
Yanga, Simba,Azam na Mafunzo bakizeni kombe la Kagame nyumbani
JULAI 14, mwaka huuu michuano ya Kombe la Kagame inatarajiwa kutimua vumbi jijini Dar es Salaam katika viwanja viwili, Taifa na Chamazi.
Yanga ni mabingwa wa tetezi wa Kombe hilo, ambao wataanza kufungua dimba kwa kucheza na Atletico ya Burundi, Simba watacheza na URA ya Uganda na Azam watacheza na Mafunzo ya Zanzibar.
Ni michuano mikubwa sana Afrika Mashariki na Kati, hivyo basi tunaziomba timu zetu ambazo zinaiwakilisha nchi katika michuano hiyo zifanye maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha wanaanza vyema michuano hiyo ili kombe libakizwe nyumbani.
Mara nyingi tumeshuhudia michuano mbalimbali imekuwa ikiandaliwa hapa Tanzania lakini matokeo yake wageni wanaondoka na kombe, hivyo hilo hatutaki litokee hata kidogo.
Tumeshaanza kuona timu zetu zikianza maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo, hivyo hiyo isiwe nguvu ya soda yawe maandalizi hasa ambayo yatawafanya wawe tishio katika michuano hiyo.
Pia makocha wa timu hizo watapata nafasi nzuri ya kuwapima wachezaji wao wapya ambao wamesajiliwa kwa ajili ya msimu huu kwa ajili ya michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Sasa basi ni wakati wa wachezaji nao kuonesha vipaji katika michuano hiyo ili kutowaangusha viongozi wenu waliofanya usajili mzuri kwa kuwaamini.
Tunazitakiwa kila la kheri timu zetu ili ziweze kulibakisha kombe hilo nyumbani.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu zibariki timu zetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment