11 July 2012

...Yaibanjua JKT Ruvu mabao 2-0



Na Mwandishi Wetu

MABINGWA Kombe la Kagame Yanga, jana waliizaba Ruvu JKT mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Licha ya JKT kufungwa mabao hayo, iliweza kucheza kandanda safi huku wakipiga pasi fupifupi wakiongozwa na mshambuliaji Hussein Bunu.


Yanga ilipata bao la kuongoza dakika ya 18 lililowekwa kimiani na Nadir Harub 'Canavaro' dakika ya 18 baada ya kukutana na mpira wa kona ulioondolewa vibaya na mabeki wa JKT Ruvu.

Katika kipindi hicho timu zote zilishambuliana kwa zamu, huku kila moja ikifanya juhudi za kutafuta mabao lakini hadi zinakwenda mapumziko Yanga ilikuwa ikiongozwa kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika ya 67, Hamis Kiiza alikosa bao la wazi baada kupewa pande zuri na Jerry Tegete aliyeingia na mpira kuanzia katikati ya uwanja.

Dakika ya 70 Kiiza alirekebisha makosa baada ya kufunga bao la pili kwa tumbo akiitokea krosi iliyochongwa na Haruna Niyonzima, ambaye alipokea pande kutoka kwa Tegete.

No comments:

Post a Comment