18 July 2012

Wanaochezea amani nchini wachukuliwe hatua haraka



JUZI Jeshi la Polisi mkoani Singida liliwafikisha mahakamani watuhumiwa wa vurugu zilizotokea wilayani Iramba na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Vurugu zilizosababisha kifo hicho zilitokea baada vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa CHADEMA uliokuwa ukifanyika Kata ya Ndago, ambapo kwa mujibu wa taarifa za polisi baadhi ya watu walianza kurusha mawe kwenye mkutano wa chama hicho kwa kile kinachodaiwa kukasirishwa na kauli zilizokuwa zikitolewa dhidi ya mbunge wao.


Lengo letu si kujadili tukio hilo, lakini kuna mambo mengi ambayo Jeshi la Polisi wanatakiwa kuyatumia kama fundisho kwenye utendaji kazi wao. Tunasema matukio ya wanasiasa kutoa matamshi ya kuudhi, lakini tunashangaa jeshi letu kukaa kimya.

Hali hiyo inaonesha wazi kuwa jeshi la polisi linahusika kufumbia macho uhalifu. Tukiachia suala Singida upo ushahidi wa wazi unaonesha matusi yanayotolewa na wanasiasa tena mbele ya watoto huku polisi wakishuhudia pasipo kuchukua hatua.

Tunavyojua kazi ya polisi ni kuzuia uhalifu usitendeke na si kusubiri ufanyike ndipo wachukue hatua. Lakini kwa hali ya sasa kuna maeneo mengine tunaweza kusema jeshi hilo linasubiri makosa yatendeke, ndipo hatua zichukuliwe.

Mifano ya hili ipo wazi na polisi hawawezi kujitenga nalo. Eneo zuri la kutolea mfano ni Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, ambapo wanasiasa walikuwa wakiporomosha matusi majukwaani huku polisi wakiangalia. Hata siku moja polisi hawakuchukua hatua.

Anayepinga hili afuatilie kauli zilizokuwa zikitolewa na Mbunge wa Mtera, Bw.Livingstone Lusinde, kwenye mikutano ya kumnadi mgombea wa CCM wakati huo. Mbunge huyo alikuwa akitoa matusi ya waziwazi mbele ya polisi, lakini hadi leo hajawahi kuchukuliwa hatua.

Tunaamini kuwa maneno yale yalikuwa ya kuudhi na yangeweza kusababisha yale yaliyotokea Singida. Tunajiuliza ni kwa nini polisi hawakumchukulie kwani maneno yalikuwa ya kuudhi.

Tuna kila sababu ya kuamini kuwa chombo hicho kingekunjua makucha yake na kusimamia sheria kwa mujibu wa katiba haya yanayofanyika sasa yasingetokea. Leo hii wanasiasa wanasimama majukwaani wanatukana huku polisi wakiangalia, haya ni mambo ya ajabu.

Tunatoa mwito kwa jeshi hilo kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, bila kujali anayevunja sheria ana wadhifa gani ndani ya jamii. Tunajua kuna watu wanajiona miungu watu wakidhani kwamba si rahisi kuchukuliwa sheria.

Tunataka Polisi ianze kuwachukulia hatua wanasiasa wanaotumia majukwaa kutoa maneno ya kuudhi ili iwe fundisho kwa wengine. Hiyo ndiyo njia pekee ya kushamirisha demokrasia kistaarabu



3 comments:

  1. NI KWELI KABISA JESHI LA POLISI LIPO KWA AJILI YA KULINDA CHAMA TAWALA AMBAO NI CCM,KWASABABU MFUMO WA UTAWALA UNARUHUSU POLISI KUPOKEA RUSHWA. KWA HIYO WANAJUA KIKIINGIA CHAMA KINGINE MADARAKANI MFUMO WAO UNAWEZA HARIBIKA NA NDIO MAANA MATUSI YALIYOTOLEWA NA WABUNGE WA CCM ARUMERU YALIKUWA SAWA ILA WAPINZANI WAKIJIBU WASHAMBULIWA NA MAWE,SASA UNATEGEMEA NINI KAMA MTU ANAKUSHAMBULIA KWA MAWE WEWE UTAJIHAMI VIPI. NA WAKATI VIJANA WA CCM WANAANZA KURUSHA MAWE MBONA POLISI HAWAKUWAKAMATA? NA NI KWANINI TU VIJANA WA CHADEMA NDIO WAKAMATWE NA WAKATI WALIKUWA WANAJIHAMI?

    ReplyDelete
  2. kwani hawa watu wa CCM Walitoka wapi kwenye mkutano wa chadema!! mi sipati jibu eti nijuzeni

    ReplyDelete
  3. TUWE WAANGALIFU NA KAULI ZA UCHOCHEZI SASA HIVI WATANZANIA WANAJICHUKUIWA SHERIA MIKONONI KILA MAHALI NI MAUAJI KITUO CHA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA WAMEACHA KUHAMASISHA AMANI WAMEKUWA WANASIASA MAUAJI YANAYOENDELEA KOROGWE KATI YA BODABODA NA MAJAMBAZI WANAOWATEKA WENYE PIKIPIKI WATU WATATU WAMEKUFA MWENDESHAJI PIKIPIKI KUUAWA NA KUWEKWA KWENYE MFUKO WA SAFETI HII IMECHOCHEA MAUAJI YA WATUHUMIWA WAWILI KUCHOMWA MOTO SHUKRANI KWA MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI ALMAARUFU MAJIMAREFU KUFIKA NA KUSHUHUDIA ISINGEKUWA ASKARI WA FFU TOKA TANGA KOROGWE INGETEKETEA MAUAJI YA KIMBARI YANGETOKEA AJABU HUTASIKIA POPOTE NI SAWA NA KUFA KWA KUKU HIZI NI ENZI ZA FREE-MASON

    ReplyDelete