18 July 2012

Wakurugenzi DECI wana kesi ya kujibu-Mahakama



Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaona washtakiwa wa kesi ya kula njama na kuiba zaidi ya sh. milioni 118 inayowakabili Wakurugenzi wa Taasisi ya Kuendesha na Kusimamia mchezo wa upatu (DECI), wana kesi ya kujibu.

Washtakiwa hao ni Bw. Dominick Kagendi, Bw. Jackson Mtares, Bw.T imotheo Loitinye na Bw. Samuel Mtares.

Hakimu Bw. Stuwart Sanga anayesikiliza kesi hiyo, aliyasema hayo jana wakati kesi hiyo ilipoletwa kwa ajili ya kutolewa uwamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.

Bw. Sanga alidai upande wa mashtaka katika kesi hiyo umeweza kuthibitisha mashtaka ya kesi hiyo hivyo washtakiwa watatakiwa kujitetea.

Hata hivyo washtakiwa hao waliiomba Mahamkama iwape muda ili wawasiliane na wakili wao waweze kujadili jinsi ya kujitetea.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidu 16 pamoja na vielelezo mbalimbali.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 20 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza utetezi.

Washtakiwa hao wanadaiwa kula njama na kuiba sh. milioni 118,440,000, mali ya DECI kupitia Benki ya Standard Chartered, tawi la Kariakoo.


No comments:

Post a Comment