16 July 2012
Wakala wa serikali toeni huduma bora kwa umma'
Na Rehema Maigala
WAKALA zilizoanzishwa na Serikali, zina jukumu kubwa la kufanikisha malengo ya Serikali, kutoa huduma bora kwa umma na kuleta mabadiliko chanya kama watatekeleza wajibu wao vizuri.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua wakazi hizo na kuongeza kuwa, lengo la kuanzishwa kwake ni kusaidia Serikali ipate muda wa kutosha kutekeleza majukumu yake ya msingi.
Majukumu hayo ni utungaji, usimamizi, utekelezaji wa sera na kuyaacha majukumu ya kiutendaji ambayo si ya lazima yafanywe ndani ya muundo wa Serikali Kuu.
Alizitaja wakala zilizozinduliwa ni Serikali Mtandao (eGa), Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Mafunzo ya Mifugo (LITA) na Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA).
“Hadi sasa tuna wakala 35 za Serikali kwa ajili ya kuleta huduma bora kwa umma na kuzingatia vigezo, Serikali kupitia utaratibu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ilifanya tathimini ya utendaji kazi wa Wakala za Serikali mwishoni mwa 2011 na kubaini uanzishwaji wa Wakala za Serikari, ulikuwa ni sahihi kwani utasaidia kutoa huduma kwa umma,” alisema.
Alisema tathmini hiyo imebaini kuwa zipo wakala ambazo mapato yao ya ndani yanaongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kubuni vyanzo vya mapato vilivyokuwepo.
Alizipongeza Wizara na wakala ambazo zimefanikiwa katika azma ya kuboresha utoaji huduma na kuongeza mapato ili ziweze zinajitegemea zenyewe.
Hata hivyo, alizitaka wakala zinazoanzishwa ziwe na tija pamoja na kuweka mkakati wa kutoa elimu endelevu juu ya dhana ya Wakala wa Serikali na lazima kuwe na mifumo thabiti ya ufatiliaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment