16 July 2012
Jaribio la kubaka lamtia matatani
Na Veronica Romwald
MKAZI wa Jangwani jijini Dar es Salaam Bw. Augustino Gasto (20), amefikishwa katika Mahakama ya Ilala kwa tuhuma ya jaribio la ubakaji.
Mbele ya Hakimu Bi. Pamela Kalala, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka Bw. Credo Rugajo, kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 6, mwaka huu, saa saba kamili mchana katika barabara ya Ocean Road karibu na hospitali ya Agakhan iliyopo Wilaya ya Ilala.
Ilidaiwa kuwa, mshtakiwa alitaka kumbaka msichana mwenye umri wa 18e. Mshtakiwa alikana shtaka hilo na alirudishwa rumande kwa kukosa wadhamini hadi Julai 25, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Wakati huo huo, Bw. Mwinyi Kombo mkazi wa Magomeni amefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma ya kukutwa ana dawa za kulevya.
Mbele ya Hakimu Bi. Janeth Kaluyende, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka Bi. Neema Haule, kuwa mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya Narcotic na paketi moja ya Heroine Julai 11, mwaka huu, maeneo ya Kariakoo wilayani Ilala.
Mshtakiwa alikana shtaka hilo na alirudishwa rumande hadi Julai 25, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment