04 July 2012

Wahamiaji wengine 42 watiwa mbaroni



Na Florah Temba, Moshi

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia wahamiaji haramu 42 kutoka nchini Ethiopia na Somalia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.


Akizungumza na waaandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz, alisema wahamiaji hao walikamatwa Julai 2 mwaka huu, eneo la Kilototoni Himo, wilayani Moshi.

Alisema wahamiaji hao waliingia nchini kinyemela kwa njia za panya na walikuwa wamejificha katika nyumba ya mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake.

Aliongeza kuwa, kukamatwa kwa wahamiaji kulitokana na taarifa zilizotolewa na wananchi ambao waliwatilia shaka watu hao. Kati ya wahamiaji hao, 39 ni raia Ethiopia na watatu kutoka Somalia


No comments:

Post a Comment