06 July 2012

Utoro wa wabunge wamkera Makinda *Asema ipo siku watakwamisha bajeti ya serikali *LHRC waponda matumizi lugha chafu bungeni



Na Benedict Kaguo, Dodoma

SPIKA wa Bunge, Bi. Anne Makinda, amewashukia wabunge wanaokimbia vikao vya Bunge na kusema kuwa, kama tabia hiyo itaendelea, ipo siku Serikali itashindwa kupitisha bajeti yake.

Bi. Makinda aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akihairisha Bunge kwa mapumziko ya mchana na kusisitiza kuwa, utamaduni wa wabunge kutoonekana bungeni na kusababisha viti vingi kuwa wazi ni wa muda mrefu.


“Wakati wa kupitia vifungu kwenye Kamati ya Matumizi ya Wizara, ni muhimi wabunge wote tuwepo, ipo siku tutashindwa kupitisha bajeti,” alisema Bi. Makinda.

Hata hivyo, tangu kuanza kwa vikao vya Bunge la Bajeti, mahudhurio ya wabunge si ya kuridhisha hivyo kusababisha wabunge wengi washindwe kuchangia.

Wakati huo huo, Waandishi Rehema  Maigala na Stella Aron, wanaripoti kuwa, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimekasirishwa na vitendo vinavyofanywa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapokuwa katika vikao vyao.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Jana, Mwanasheria wa LHRC, Bi. Imelda Urio, kwa niaba ya Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt. Hellen Kijo-Bisimba, alisema wabunge wanafanya mambo ambayo ni kinyume na katiba ya nchi.

“Mambo ambayo hatufurahishwi nayo ni pamoja na matumizi ya lugha chafu, zile za kuudhi na matumizi ya kanuni namba 64 (1), inayowatoa wabunge ndani ya ukumbi.

“Pia kuna tatizo la kutawala kwa itikadi za vyama vya siasa badala ya kutanguliza masilahi ya Watanzania, mara nyingi tumeona wabunge wakizomeana kuhusu jambo fulani,” alisema Bi. Urio na kuongeza kuwa, kituo hicho pia kimebaini mahudhurio hafifu ya wabunge wakati wa majadiliano ya bajeti.

“Wabunge wetu wanapoteza muda mwingi ambao ni wa thamani kwa kuomba mwongozo na taarifa hivyo kusababisha fujo bungeni, wanapochangia hoja hawatumii muda huo vizuri zaidi ya kutoa maneno ya kejeli na kuudhi badala ya kujikita katika bajeti.

“Salamu za pongezi na pole zinaendelea kutolewa kinyume na kanuni namba 151(1)-(4), kitu ambacho anatakiwa kutoa kutoa spika wa bunge pekee, uwiano wa fursa sawa katika mijadala ya bajeti imekuwa ukitolewa kwa upendeleo, zipo tuhuma kwa viongozi ambao wanaongoza vikao vya Bunge kuwa na upendeleo wakati wa kuwasilisha hoja mbalimbali,” alisema.

5 comments:

  1. Huyo mwanamke hawezi uongozi angechaguliwa mwingine.Maana anapendelea chama cha ccm ambacho kilimuweka uspika,hawezi kwenda kinyume other wise wata Mlimboka.

    ReplyDelete
  2. WANAFIKIRI KUNA UPENDELEO NI WENYE UFINYU WA WAKUONA MBALI KINACHOFANYIKA BUNGENI NI SAWA NA COMEDI INASIKITISHA FEDHA CHACHE KODI ZA WATANZANIA ZINATUMIKA KURUSHA VIPINDI VYA BUNGE SAWA NA COMEDI BADALA YA KUONYESHA VIPINDI VYENYE TIJA HAINGII AKILINI WABUNGE WANAISIMAMIA SERIKALI ITIMIZE WAJIBU WAKE KILA SHUGHULI "VALUE FOR MONEY" MBONA WANATOROKA BUNGENI LAKINI WANASAINI POSHO SPIKA HAWEZI ACHAGULIWE ATAKAYEBADILI ORDER PAPER WAJADILI MAJUNGU KITUO CHA HAKI ZA BINADAMU KIBADILISHWE JINA HIKI NI CHAMA CHA UPINZANI KISICHOTAKA KUSAJIRIWA UKO UKIUKWAJI MKUBWA WA HAKI ZA BINADAMU HAUKEMEWI SASA HIVI NI KAMPENI ZA SIASA

    ReplyDelete
  3. NIMEFURAHISHWA NA UENDESHAJI WA BUNGE WA MAMA MAKINDA KWENYE BUDGET YA UJENZI NA MAWASILIANO WABUNGE WOTE WALIIJADILI KWA NIDHAMU YA HALIYA JUU WAKATI WA KUPITISHA VIFUNGU WALIWEZA KUPITIA VITABU VYOTE TOFAUTI NA WENGINE NIKUOMBE SPIKA ENDELEA KUONYESHA NJIA KWA VITENDO NA USHAURI WABUNGE WAPEWE SEMINA AMBAYE HATABADILIKA TUTAMSUBIRI MWAKA 2015 TUTAKUTANA NAYE KWENYE SANDUKU LA KURA

    ReplyDelete
  4. Kuna shida katika uongozo wa hili bunge dats why wanatoroka wengi si kawaida... Tatizo wanalijua wenyewe ila wanavunga tuu.

    ReplyDelete
  5. kwani haiwezekani kuwa mbunge ambaye hajafika kuhudhuria vikao vya bunge...kwa hiyo cku bila taarifa zozote kwa katibu wa bunge....naomba acmamishe vivyo hivyo kuhudhurunze vika vitano ili wajifunze...kwan waendeleeizama kutizama luninga majumbani kwao...............ni hayo 2 mi nazama kama spika hatocmamia kanuni na taratibu za bunge...eti mpaka aridhie hatutofika kabisa

    ReplyDelete