09 July 2012

TBF yampongeza Thabit kujiunga Oklahoma



Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF),  limempongeza Mtanzania Hashim Thabit anayecheza mpira wa kikapu Marekani kuingia mkataba wa miaka miwili na timu  ya Oklahoma City Thunder.

Akizungumza kwa simu akiwa jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti TBF,  Phares Magesa alisema ni wakati sasa wa kujivunia mafanikio ya baadhi ya watanzania wanaofanya vizuri katika viwango vya kidunia kwani ni historia ya michezo huo tangu upatikane uhuru.

Alisema Thabit ni mchezaji pekee aliyeweza kufanikiwa na kucheza ligi ya juu kabisa duniani katika michezo huo.

Alisema wapo watanzania wengi wamefanikiwa katika michezo mbalimbali ila kila mchezo una ligi zake ambazo ni za kiwango cha juu.

Alisema kwa upande wa wa Thabit yeye pekee ndio ameweza kufanya hivyo kwa kufanikiwa kucheza mfululizo ligi hiyo kubwa Duniani.

Kabla ya timu hiyo Hasheem amecheza timu za Memphis na baadaye kucheza Houston Rockets na mwshoni mwa msimu uliopita alicheza Portland Trail Blazers.

Alisema Katika timu ya Blazers alicheza michezo yote 16 liyokuwa imebaki kabla ya msimu kumalizika.

Alisema Hasheem kwa sasa ndio mwafrika mwenye kiwango cha juu kabisa miongoni mwa waafrika wanaocheza kikapu Marekani na ni mchezaji pekee anayecheza huko toka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Kusini.

Alisema Kwa Hasheem kuchukuliwa na timu kama Oklahoma City ambao ni mabingwa wa Kanda ya Magharibi ya NBA na mwaka huu walicheza fainali ya ubingwa wa NBA na kushindwa na Miami Heat, inaonyesha anathaminiwa na bado ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kubwa kama OKC ili iweze kufikia malengo yake.

No comments:

Post a Comment