17 July 2012
Sita kortini wakidaiwa kumuua M/kiti CCM
Na Damiano Mkumbo, Singida
WATU sita jana wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida kujibu mashtaka ya tuhuma za mauaji ya Katibu wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Ndago, marehemu Yohana mpinga (31), yaliyotokea juzi mjini hapa.
Washtakiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Bi. Ruth Massamu ambao ni Manase Daudi (40), William Elia (33) Charles Leonard (20), Frank Stanle (31), Philipo Edwad (30) na Titho Nitwa (37).
Mwananasheria Mwandamizi wa Serikali, Bi. Neema Mwanda, alidai washtakiwa hao wanadaiwa kumuua marehemu baada ya vurugu zilizotokea katika mkutano wa hadhara ambao uliandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenye Kijiji cha Nguvumali, saa 10 jioni, Julai 14 mwaka huu, saa
Katika kesi hiyo, washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kuendesha kesi ya mauaji hadi Mahakama Kuu. Kesi hiyo imehairishwa hadi Julai 30 mwaka huu.
Wakati huo huo, Ofisa wa Sera na Utafiti, Makao Makuu ya CHADEMA, Bw. Mwita Waitara, jana alifikishwa katika Mahakama hiyo kwa tuhuma ya kutoa lugha ya matusi katika mkutano wa chama hicho uliofanyika Julai 14 mwaka huu.
Bw. Waitara anadaiwa kutoa matusi yaliyomlenga Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Bw. Mwigulu Nchemba lakini alikanusha madai hayo na kupewa dhamana. Kesi hiyo itaendelea Julai 30 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment