09 July 2012

Simba, Azam zadaiwa kupanga matokeo



Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MADAI ya upangaji matokeo ili Azam FC na Simba SC zicheze fainali ya Kombe la Urafiki Tanzania, umewakwaza makocha wa timu zinazoshiriki mashindano hayo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa.


Hali hiyo ilidaiwa kusababisha na Yanga baada ya kuondolewa kwenye mashindano hayo, mechi za Simba na Azam FC zimekuwa mechi pekee zikiingiza mashabiki kwa kiasi kidogo kuliko ilivyokuwa kwenye mashindano ya
Kombe la Mapinduzi.

Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya makocha wa timu zilizoshoriki mashindano hayo kwa kusema upangaji huo matokea hauwasaidii na unazidi kudidimiza soka la Tanzania.

"Wangeacha atakayeshinda acheze fainali lakini kwa aina hii ya kupanga timu fulani inatuumiza na kutupotezea muda kwa kuwa tumejiandaa lakini mwisho yanatokea mambo tofauti", alisema mmoja wa makocha ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini.

Walisema tatizo hilo ni kwa timu za Zanzibar lakini timu kutoka bara wanazichukulia kama kitu kikubwa lakini ukija uwanjani wanakuwa sasa na wakati mwingine timu za visiwani zinaonesha kiwango kizuri.

Mashindano hayo yamepoteza radha, mvuto na hamasa kutokana na mashabiki wachache wanaoingia uwanjani hasazinapokutana timu za kutoka visiwani hapa.

No comments:

Post a Comment