04 July 2012
Serikali yafafanua taratibu za kuongoza vyuo vikuu
Na Pendo Mtibuche, Dodoma
SERIKALI imesema haianzishi Vyuo Vikuu ili kuongeza idadi ya wanafunzi bali kwa madhumuni maalum.
Niabu Waziri wa Elimu nmu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Muyuni, Bw. Jaku Hashimu Ayoub.
Bw. Ayoub alitaka Serikali ifafanue ni lini itajenga Ofisi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi pamoja na vigezo ambavyo vinatumika kujenga Vyuo Vikuu upande mmoja wa Muungano.
Akijibu swali hilo, Bw. Mulugo alisema Zanzibar kuna Vyuo Vikuu vya Umma vitano ambavyo kati ya hivyo viwili vya binafsi wakati Bara kuna Vyuo Vikuu 11 vya umma na binafsi 34.
Alisema uanzishwaji wa Vyuo Vikuu unategemea uwezo wa kifedha wa Serikali lakini kwa kiasi kikubwa, sekta binafsi zinamchango mkubwa kukuza elimu kwa pande zote za Muungano.
Aliongeza kuwa, uanzishwaji wa vyuo hivyo unategemea uwepo wa wadau, wanafunzi wenye sifa, rasilimali watu, maji, wahadhiri, miundombinu, vifaa vya kufundishia, kujifunzia na madhumuni halisi ya kuanzishwa Chuo Kikuu husika.
“Kwa mantiki hii, Vyuo Vikuu havianzishwi ili kuongeza idadi ya wanafunzi bali kwa madhumuni maalumu kulingana na mahithalisi, uanzishwaji wa Ofisi ya Bodi ya Mikopo Zanzibar, umekamilika na imeanza kazi Aprilimwaka huu,” alisema .
Wakati huo huo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Bw. Ally Kessy, alisema jimbo lake lina watu wanaofikia milioni 1.6 ambao ni wengi kuliko wananchi wa Zanzibar.
Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali haioni umuhimu wa kujenga Ofisi ya Bodi ya Mikopo ili wananchi wa maeneo hayo wasipate adha ya mikopo.
Akijibu swali hilo, Bw. Mulugo alisema hivi sasa Serikali imeweza kujenga ofisi katika mikoa ya Dar es Saalam na Dodoma na ina mpango wa kuwa na ofisi zingine Mwanza, Arusha na Mbeya.
Alisema hadi sasa, Serikali hajipata usumbufu wa utoaji mikopo kwa wanafunzi katika ofisi hizo kwa kuwa inatumia mtandao wa kompyuta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment