16 July 2012

Mwanza yatinga fainali Copa Coca-Cola


Na Janath Abdulrahim

TIMU ya Mwanza imetinga fainali ya michuano ya vijana wenye umri wa miaka 17 (Copa Coca-Cola) baada ya kuichapa Temeke kwa mabao 3-1 katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulioanza saa 2 asubuhi, timu zote zilianza kwa kasi ambapo Mwanza iliwachukua dakika tatu kufunga bao la kwanza, lililofungwa na Jamal Mtegeta.


Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu ambapo mpaka dakika 45 za kwanza zikimalizika, Mwanza iliongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kazi ambapo Temeke ilijipanga na kusawazisha bao hilo dakika ya 55, kupitia kwa Baraka Mtarukundo na kufanya mpaka dakika 90 zikimalizika timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Kutokana na matokeo hayo, ziliongezwa dakika 30 za ziada ambapo Mwanza ilijipatia bao la pili dakika ya tano lililofungwa na Mtegeta na dakika ya 20, Dickson Ambundo alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu.

Mwanza sasa inamsubili mshindi kati ya Morogoro na Tanga ambapo fainali inatarajiwa kupigwa kesho kwenye uwanja huohuo.

No comments:

Post a Comment