05 July 2012

Milovan atambia silaha zake mpya



Na Speciroza Joseph

BAADA ya kuanza vizuri mashindano ya Urafiki Tanzania, kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic ameridhishwa na kiwango cha wachezaji wapya waliojiunga na timu hiyo.

Akizungumza na gazeti hili visiwani humo,  Milovan alisema timu yake inawachezaji wengi wapya ambao mwanzo ilimpa wakati mgumu lakini sasa wameanza kuelewana na kufanya vizuri kwenye michezo mbalimbali.

Alisema hadi kufikia mashindano ya kombe la Kagame wachezaji wake watakuwa katika kiwango kizuri kitakachosaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano hayo na ligi kuu msimu ujao.

Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji hao wameweza kucheza bila kuwepo kwa wachezaji muhimu katika timu hiyo kama Haruna Moshi 'Boban' hivyo atawatumia kwenye mashindano ya Kagame pia.

"Ni muda mchache wameonesha kiwango kizuri, wamecheza vizuri natumaini watafanya zaidi ya hapa kwa mazoezi watakayopata kabla ya kuanza ligi kuu" alisema  Milovan.

Alisema michezo ya mashindano hayo yatakuwa sehemu ya kupima wachezaji wake na kupata timu imara itakayoleta ushindani kwenye michuano ijayo.

No comments:

Post a Comment