23 July 2012
Michuano ya IDFA kuzinduliwa leo
Na Daud Magesa, Mwanza
MICHUANO ya Kombe la Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilemela (IDFA), Mwanza itazinduliwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza.
Michuano hiyo imerejeshwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), baada ya kusimama kwa kipindi kirefu, ambapo itashirikisha timu 24 kutoka wilayani humo, vyenye usajili na visivyosajiliwa na Msajili wa Klabu na Vyama vya Michzo nchini ili kukuza vipaji vya wachezaji .
Katibu Mkuu wa IDFA, Juma Msaka akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, alisema michuano hiyo imelenga kukuza vipaji vya wachezaji wanaochipukia wilayani humo na ambao hawajapata nafasi kuonesha uwezo wao.
Alisema Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza amepewa jukumu ya kuzindua michuano hiyo ambayo itachezwa kwa mtindo wa mtoano, ambapo timu bingwa itajinyakulia kitita cha sh. 500,000, wa pili sh. 300,00 na wa tatu sh. 250,000. Timu sita bora zitazawadiwa seti moja ya jezi na mpira kila moja.
“Tumepokea kalenda ya matukio ya TFF ikionesha kurejesha mashindano ya FA na tunawajibika kutekeleza maagizo hayo. Kamati ya Utendaji ya IDFA, imeridhia kufanyika kwa michuano hiyo Julai 21 hadi Agosti mwaka huu, ambapo itazinduliwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,” alisema Msaka.
Alisema katika mchuano hiyo wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 na wale wa Ligi Kuu hawataruhusiwa kucheza katika mashindano hayo, yatakayodumu kwa wiki mbili na kuiomba TFF kubadili kanuni zake kuwazesha wachezaji hao kushiriki mwakani.
Msaka alisema kuwa kabla ya mashindano hayo ambayo yamepangwa kuchezwa kwenye viwanja vitatu vya Magomeni, Buswelu na Airport, kutafanyika maandamano kwa timu zote ambayo yataanzia Uwanja wa Furahisha kupitia mitaa ya Penda, Kitangiri, Bomani na kumazilikia Uwanja waa CCM Kirumba.
Alisema baada uzinduzi huo kutachewaa mechi moja kati ya timu ya Beach Boys ya Kirumba Mwaloni dhidi ya timu ya wauza mbao wa Saba Saba (Mbao FC), ambapo michuano hiyo itaendelea Julai 22.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment