23 July 2012

Toto African yawaomba radhi wapenzi wa soka



Na Daud Magesa, Mwanza

UONGOZI waa Klabu ya Toto African, imewaomba radhi wadau, wapenzi wa soka na vyama vya mchezo huo kutokana na kugomea mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba hivi karibuni.

Baadhi ya viongozi wa timu hiyo inayoshiriki Lig Kuu Tanzania Bara, wanadaiwa kugoma timu isishuke uwanjani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba ambayo ilikwenda kulitembeza Kombe la Ligi Kuu baada ya kulinyakua.


Viongozi hao wanadaiwa kushinikiza waandaaji wa mechi hiyo kuwalipa sh. milioni 2, kinyume cha makubaliano na kusababisha kuchelewa kuaanza kwa mechi hiyo.

Kutokana na kadhia hiyo jana viongozi hao waliomba radhi kwa wadau, wapenzi wa soka  na vyama vya mpira wa miguu vya wilaya na mkoa kutoka na kitendo hicho.

Akiomba radhi kwa niaba ya uongozi wa Toto mbele ya waandishi wa habari jijini hapa jana, Meneja wa timu hiyo Beatus Madenge, alikiri kufanya kitendo hicho ambacho kiliwakwaza wapenda soka jijini hapa na nje ya jiji ambao walijitokeza kushuhudia mchezo huo ambao Toto ilifungwa mabao 2-0.

“Kwa niaba ya uongozi wa Toto, tunaomba radhi kama binadamu tuliwakwaza sana wadau wetu, wapenzi na viongozi wa Serikali ya Mkoa pamoja na vyama vya soka.

"Si kwamba tuligomea timu isiingie uwanjani kucheza na Simba hadi tulipwe fedha, hapana wachezaji walichelewa kupata chakula ndiyo sababu ya timu kuchelewa kuingia uwanjani, hili tunaahidi halitrudiwa tena tuomba mtuwie radhi,” alisema.

Katika mchezo huo ambao uliandaliwa na Kampuni ya World Wide Entertainment, wadau wa soka na viongozi soka na serikali, walilaani kitendo hicho kinachodaiwa kufanywa na watu wachache ndani ya klabu hiyo kwa maslashi yao.

No comments:

Post a Comment