02 July 2012
Mfanyabiashara akutwa amefariki ndani ya gari lake
Na Neema Malley
MFANYABIASHARA Bw.Edward James (67) amekutwa akiwa amefariki dunia akiwa kwenye gari lake nje ya hotel ya Protea.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Bw. Chales Kenyela alisema kuwa mEI 28 mwaka huu barabara ya Ally Hassan Mwinyi marehemu alikutwa kwenye hotel ya Protea amekufa huku akiwa ameketi kwenye gari yake.
Kamanda Kenyela alisema kuwa kutokana na maelezo yaliyotolewa na mtoto wa marehemu Bw. Sema Mwaipungu(32) alisema kuwa marehenu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na alishafanyiwa oparesheni nchini Uingereza.
Pia aliongeza kuwa marehemu alikuwa anatarajiwa kurudi nchini humo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na upelelezi unaendelea kufanyika.
Katika tukio lingine mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Bw.Peter Ramadhani aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (20-25) alikutwa akiwa amefariki ufukweni mwa bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 28 saa 10 maeneo ya Mbweni ufukweni mwa bahari ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amefariki.
Kwa mujibu wa Bw. Isaac Hamad (18)ambaye ni mvuvi na ni mkazi wa Pemba alisema kuwa siku ya tukio saa nne asubuhi walikuwa pamoja na marehemu baharini wakivua samaki.
Bw. Hamad alisema kuwa baadae yeye aliondoka na kumuacha marehemu ndani ya chombo akidai anasubiria hadi maji yapungue hatahivyo ilishindikana ambapo maji yalimzidi na kumsababishia kuzama na mwili wake kuokotwa eneo hilo.
Kwa mujibu wa kamanda Kenyela mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na upelelezi unaendelea kufanyika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment