06 July 2012

Mchora katuni bora kuibuka na dola 1,500



Na Mwandishi Wetu

MSHINDI wa kwanza katika mashindano ya kutafuta mchora katuni 'kibonzo bora', kitakachoelezea changamoto za kibiashara zinaozikabili nchi atanyakulia dola za Marekani 1,500.

Jumla ya zawadi zilizotengwa kwa washindi sita kati ya 20 katika maonesho hayo ni dola 4,000 za Marekani.


Kazi za wachora vibonzo hao sita zimechapishwa kwenye ripoti itakaiyotolewa katika onesho litakalofanyika leo kwenye Ukumbi wa Nafasi Art Space, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Lengo la onesho hilo ni kuelezea ripoti ya vikwazo vya biashara nchini iliyoandaliwa na mshauri mwelekezi wa Uingereza, David Irwin na kutolewa na Kitengo cha Utetezi cha Mpango wa Kuimarisha Mazingira ya Biashara Tanzania 'BEST-AC'.

Vikwazo kwa biashara ambavyo vimeainishwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na umeme, miundombinu ya barabara, rushwa na maji na vitaoneshwa na wachoraji wa vibonzo ambao walishiriki katika mashindano yaliyojikita
kwenye vitu ambavyo, viongozi wa kibiashara wameanisha kuwa vikwazo vikuu katika kufanya biashara nchini.

Ripoti hiyo imeandaliwa na jumuiya tatu za biashara nchini ambazo ni Shirikisho la Biashara na Viwanda (CTI), Shirikisho la Utalii Tanzania (TCT) na Jumuiya ya Vikundi vya Biashara Ndogondogo (VIBINDO).

Akizungumza Dar es Salaam juzi Mwenyekiti wa VIBINDO, Gaston Kikuwi alisema Watanzania ikiwa ni pamoja na watendaji wa biashara, watapata fursa ya kuburudika na masihara kuhusu vikwazo vya biashara nchini na kutafakari hatua za kuchukua.

“Ni matarajio yangu kwamba shughuli kama hii itawafanya wadau wote kuongeza bidii ya kuboresha mazingira ya biashara,” alisema.

Kwa mujibu wa Rachel Kessy, mratibu wa mashindano hayo, ambaye pia ni msimamizi wa Music Mayday Youth Centre, alisema michuano ya uchoraji vibonzo ilikuwa mikali hadi kufikia kupatikana kwa washindi hao.


No comments:

Post a Comment