06 July 2012

Kilango aishukia serikali


Na Benedict Kaguo, Dodoma

KAMATI ya Bunge ya Miundombinu, imeshangazwa na hatua ya Serikali kuacha kufikiri mipango ya kwenda mbele kuhusu ujenzi wa barabara katika Jiji la Dar es Salaam badala yake imekuwa ikifanya maamuzi yanayoirudisha nchi miaka 36 iliyopita.


Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bi. Anne Kilango Malecela, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa mwaka wa fedha 2011/12 na maoni ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya matumizi ya Wizara ya Ujenzi mwaka 2012/13.

Alisema mwaka1976 wakati Jiji la Dar es Salaam likiwa na watu wachache, eneo kubwa likiwa pori ambayo Hayati Mwalimu Julius Nyerere alijenga barabara ya Mandela yenye njia mbili.

“Mheshimiwa Spika, leo hii bado tunaendelea kujenga barabara za njia mbili maana yake ni kwamba, mawazo yetu hayaendi mbele yanarudi nyumu,” alisema Bi. Malecela.

Alisema kutokana na hali hiyo, kamati hiyo inashauri barabara zote za Dar es Salaam ikiwemo ya Kilwa, Morogoro, Nyerere, Bagamoyo na Mandela, zipanuliwe na kuwa za njia nne.

Alisema kamati inashauri kuwa Serikali inapopanga kujenga barabara ifikirie miaka mingi ijayo badala ya kujenga pana
zitakazohimili wingi wa magari kwa miaka mingi mbele.

Akizungumzia tatizo la msongamo wa magari Dar es Salaam, Bi. Malecela alisema kamati inashauri Serikali itatue kero hiyo kwa kujenga na kuimarisha barabara za pembezoni, kujenga barabara za juu, kuweka usafiri wa reli na boti kutoka Bagamayo hadi Feri.

Wakichangia hotuba hiyo, baadhi ya wabunge walitaka kasi zaidi ya ujenzi wa barabara hasa za mikoa ili kupunguza tatizo la mfumko wa bei za vyakula.

Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM) Dk Haji Mponda alisema ili kuondokana na tatizo la mfumko wa bei za vyakula vema serikali ikawekeza katika kuboresha barabara za vijijini ambapo ndiko chakula kinakotoka kwa wingi.

Mbunge wa Kyerwa, mkoani Kagera, Bw. Eustace Katagira (CCM), aliitaka Serikali kutimiza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete kujenga barabara ya Karagwe-Kyerwa hadi mpaka wa Uganda ili kuchochea kasi ya maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Alisema kwa muda mrefu barabara hiyo imekuwa ya udongo ambapo wakulima wanapata tabu kusafirisha bidhaa zao za kilimo ikiwemo Kahawa kwenda katika masoko ya nchi jirani ya Uganda na kwingineko.


2 comments:

  1. NYERERE ALIONGOZA TANZANIA KATIKA KIPINDI KIGUMU RASILIMALIWATU WALIKUWA WACHACHE LAKINI HATA WALE WALIOCHAGULIWA HAWAKUWA "COPY AND PASTE"IS INASHANGAZA UPEO ANASIMAMA MBUNGE KULAANI WAAFRIKA KUWA NI WAVIVU WA KUFIKIRI AKITUKUZA WAZUNGU AMESAHAU KUWA WAKATI WAAFRIKA WAKIJENGA MAPIRAMID KULE MISRI WAZUNGU WALIKUWA MAPANGONI NIMECHUKIA KAULI YA MBUNGE WA IRINGA MJINI KUTUKUZA WAZUNGU NA KUTUKANA WAAFRIKA HUYU NI KIBARAKA WA WAKOLONI SIMTOFAUTISHI NA MWANASHERIA WA KENYA CHARLES MUGANE NJONJO MIAKA YA 1963- 1979 ALIKUWA HAAMINI KUPANDA NDEGE ILIYOENDESHWA NA MTU MWEUSI HUYU NI MPUMAVU SAWA PIA NA MANGOSUTHU BUTHELEZI KIONGOZI WA WAZULU "INKATHA FREEDOM PARTY MIAKA YA 1975 AKISHIRIKIANA NA MAKABURU KUMPINGA NELSON MANDELA HUYU NI KIBARAKA PIA. WABUNGE WANAKOSOA SANA BILA KUPENDEKEZA HATUA ZA UFUMBUZA MTAZAMO NI WA KI-IDEALIST DHANIFU KULIKO KI-REALISTIC [SCIENTIFIC] UHALISIA .WANANIFU WAKIPEWA SERIKALI BADALA YA KUAMBIA WATU WAFANYEKAZI WAO WATAWAAMBIA WAFUMBE MACHO WASALI WAPATE MIUJIZA HAWA NI AKINA MCHUNGAJI MSIGWA WAACHE KUDANGANYA WATANZANIA WANA UTUMWA WA MAWAZO MBAYA KULIKO UTUMWA WA MWILI

    ReplyDelete
  2. Hivi hii serikali yatanzania itafunguka lini,na wanapeleka wapi pesa za walipa kodi. Angalia mfano Kenya tu sasa barabara za nairobi wanatengeneza fourways na wanaanza kutengeneza flyovers. Sijui hawa wabunge. Na mawaziri wana kazi gani.... Wapuuzi tu kwa hii kasi yao ya konokono Tanzania haitaenda kokote

    ReplyDelete