11 July 2012
Dkt. Slaa amjibu Waziri Nchimbi *Asema liwalo na liwe, hawaweze kuhojiwa na polisi *Wadai Idara ya Usalama ndio inastahili kuchunguzwa
Na David John
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibroad Slaa, amesema pamoja na madai waliyotoa kwa Serikali juu ya kuandaa mkakati wenye lengo la kuwateka, kuwadhuru baadhi ya viongozi wake kitaifa, hawapo tayari kuhojiwa na Jeshi la Polisi kama alivyoagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Alisema msimamo huo unatokana na chama hicho kutokuwa na imani na jeshi hilo ambalo kwa nyakati tofauti, limeshindwa kushughulikia malalamiko ya chama hicho ambayo wamekuwa yakiyapeleka kwa masilahi ya Taifa.
Dkt. Slaa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari siku moja baada ya Dkt. Nchimbi, kuliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji baadhi ya viongozi wake waliodai Serikali imeanda mkakati huo ambao unaratibiwa na Usalama wa Taifa.
Mbali ya Dkt. Slaa, viongozi wengine waliodai kuandaliwa mkakati huo ambao Dkt. Nchimbi, aliagiza wahojiwe na polisi ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbress Lema na Mbunge wa Ubungo, Bw. John Mnyika.
“Tumechoshwa na tabia ya Jeshi la Polisi kupuuza malalamiko mbalimbali ambayo tunawapelekea juu ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo yanayogusa masilahi ya Taifa hivyo hatupo tayari kuhojiwa wala hatuoni sababu ya kujipeleka vinginevyo tupo tayari kukamatwa,” alisisitiza Dkt. Slaa.
Alisema Kamati Kuu wa CHADEMA ambayo ilikutana jana, ililaani hatua ya viongozi wake kupokea vitisho ambavyo vinahatarisha usalama wa maisha yao.
Aliongeza kuwa, pamoja na vitisho hivyo, tayari amepokea simu kutoka kwa mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa Ofisa wa Polisi kutaka akutane naye.
“Nilichomwambia ni kwamba, sina muda huo na sipo tayari kukutana naye wala mtu mwingine yeyote,” alisema Dkt. Slaa akipinga agizo la Dkt. Nchimbi, kutaka polisi iwahoji.
“Dkt. Nchimbi hakustahili kutoa agizo kama hili badala yake wao walipaswa kuichunguza Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi ndiyo maana Wizara hii inapewa bajeti kubwa kwa ajili ya mambo kama haya.
“Wizara hii inatengewa fedha nyingi kwa ajili ya mambo kama haya hivyo lazima yachunguzwe kwa kina badala ya kutoa kauli zisizo na tija, umaaarufu wa chama chetu na sisi wenyewe hautokani na siasa bali ni kukubalika na wananchi si vinginevyo,” alisema Dkt. Slaa.
Katika hatua nyingine, chama hicho kimetangaza ratiba yake ya kujikita katika mikoa mitano siku 44 kwa ajili ya kujiimarisha na kuhamasisha wananchi kukiunga mkono.
Alisema mikutano hiyo imepewa jina la “Operesheni Sangara” chini ya kauli mbiu inayosema; “Hakuna kulala, hakuna kula, hakuna kunywa hadi kieleweke”.
Dkt. Slaa alisema miongoni mwa mikoa inayolengwa kwenye operesheni hiyo pamoja na Singida, Dodoma, Tabora, Shinyanga na watafika vijiji 4,000, kata 806 na majimbo 44, kwani lengo cha chama hicho ni kuongoza Serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SIAMINI KUWA KUNA MTU ALIYE JUU YA SHERIA HII TANZANIA NI YETU WOTE NI WEHU NYUMBA UNAMOLALA NA FAMILIA YAKO KUIMWAGIA PETROLI UKIFIKIRI WEWE HUTADHURIKA KILA MTU AKINYAMAZA KIMYA WATU WWOTE HUONEKANA WANA BUSARA ILA WAKIZUNGUMZA NI RAHISI KUWATOFAUTISHA TABIA
ReplyDeletenafikiri busara zaidi itumike kuliko jazba kwani wana siasa mkiendelea kulumbana kusiko faida kwa maslahi ya taifa mwisho ni mahakama kwa ajiri ya waafrika HAGUE
ReplyDeleteHivi ninyi watanzania,nani amchunguze mwizi mwenzake,nani amchunguze gaidi mwezake,nani amchunguze fisadi mwezake,polisi amchunguze polisi mwezake,usalama wa kikwete uchunguze usalama wa kikwete.Siyo usalama wa Taifa bali wa Kiwete na Mtoto wa mkuluma (mtoto wa Riwalo na liwe).Hii haipo nidanganya toto.Wanavo uambona wanageuza ripoti.Nani hawaamini?????Huenda mizimu.Serikali mbovu haiwezi kujichunguza.Pole sana.Siku inakuja ambayo siyo mbali ccm na serikali yake iondoke na viongozi wote watiwe ndani.Riwalo na LIWE
ReplyDeleteHIVI IKITOKEA CHADEMA IMESHIKA NCHIWATAPATA WAPI ASKARIPOLISI,WANAJESHI,MAAFSA USALAMA WATAIFA,MAJAJI .HAINGII AKILINI KUJIONA WAO WAMEJAZA RASILIMALIWATU KWAMBA WENZAO NI MAZUZU .MWISHO WA UONGO NA UZUSHI UTAFIKIA PALE UKWELI UTAKAPOWEKWA HADHARANI MUNGU HAMFICHI MNAFIKI
ReplyDeleteSUBIRI KWANZA WASHIKE NCHI NDIYO UTAJUA.UNYANYASAJI NA MATUMIZI MABAYA YA VYOMBO VYA DOLA YATAKOMA NA MAFISADI WATAKIONA CHA MTEMA KUNI
DeleteHUO NI UPUUZI WA DR SILAHA.
DeleteANA MAANA AKISHIKA URAIS ATAWAFUKUZA KAZI ASKARI WOTE, MAHAKIMU WOTE, MAJAJI WOTE NA MAAFISA USALAMA WOTE NA KUAJIRI WAKWAKE?
aCHA USANII WA KISIASA SILAHA
Tupelekeni pole pole demokrasi ndo itaamua hatima ya nchii hii
ReplyDeleteSIO SIFA KUKAIDI VYOMBO VYA DOLA TUHUMA ZISIZO NA USHAHIDI ZISIPOCHUNGUZWA KWA UANGALIFU BAADAYE NI WATU KUSHITAKIWA KWENYE MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUNA WAKATI CHADEMA WALITUHUMIWA KUMUUA CHACHA WANGWE WA CHADEMA JE TUHUMA ZIMEISHIA WAPI????? TUCHUNGE MIDOMO YETU SI VEMA MDOMO UKUTAWALE KAMA UMEUAZIMA NA UNAKIUKA MATAKWA YAKO KUZUNGUMZA BILA KURUHUSIWA URUDISHE KWA MWENYEWE UNAKUFANYA UONEKANE KICHAA
ReplyDeleteWAACHE UZUSHI,CHADEMA WANABWABWAJA MNO!!! MANENO MENGI SIO UONGOZI!! NA HAWATASIFIWA KWA UONGO WAO,INAONYESHA HATA SEREKALI YAO ITAKUWA YA KUZUA MAMBO TU!JESHI,POLISI,TISS,MAHAKAMA N.K HAWAVIAMINI WAKIINGIA MADARAKANI WATAKUWA NA VYOMBO VYAO? WAJITAHIDI KM WATAWEZA JAPO NAJUA NI VIGUMU,WAKIAMINI KILA CHOMBO.AU WANATAKA WAKIINGIA MADARAKANI USALAMA WA NCHI WATAAJIRI WAZUNGU NDO WAWE WANAWAPA HABARI? NA MBIU YAO YA PEOPLES POWER NI WANANCHI KWA UJMLA WAO,SIO CHAMA KM CHAMA KINAWEZA KUITUMIAWANANCHI WAKIAMUA WANAWEZA KUITUMIA BIU HIYO HATA DHIDI YAO! WASOME KOTE ILIKO TUMIKA NA WAONE MADHARA YAKE!!! WASIWE KAMA MBAYUWAYU HATA HAO AKINA MBOWE,SILAA WANA MAOVU YAO SI WASAFI HIVYO!!!
ReplyDeletemimi naonaboramafisadi waccm.yameshashiba tunaweza kupumua.tukiwachagua hawa SILAA BUNDUKI,MBOWE,nahawa wadogowaogo mbonatutakonda,kwasababu mpakawamalize migolofayao tumekuwashindano.
ReplyDeleteYOTE YANA MWISHO KAZI KWENU!
ReplyDeleteHata washabiki wa kuandika habari wapo, serikali chafu huonekana hadharani madhambi yake, Ni kweli vyombo vya usalama wa taifa na polisi hivi sasa vinatumika vibaya hasa vinapofanya kazi za binafsi vinaaacha kazi ya umma ni makosa kabisa, mifano imeonekana kuhusu na kupigapiga wananchi,wanafunzi vyuoni na ukatiri wa kulinda wawekezaji kinyume na kazi yake ya kuundwa/kuanzishwa,kuzuia maandamano kwa visingizio vya kutokea vurugu,na visingizio vingine kemukemu, hii ni hatari kwa wanajamii kuwajengea usugu halafu unategemea amani ya mdomo.
ReplyDeleteSHAARAP! Nimeshakuona Wewe ni CHADEMA na una tamaa ya FISI
Delete