05 June 2012

Timu ya riadha DAA imeiva kimashindano

Na Andrew Ignas


KAMATI ya utendaji ya Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es salaam(DAA),imesema kikosi cha timu ya riadha kinaendelea vizuri na mazoezi.

Akizungumza  Dar es salaam jana Katibu wa chama hicho Lucas Nkungu, alisema kikosi cha timu ya Riadha ya Mkoa wa Dar es salaam kinaendelea kujinoa vyema kwaajili ya kuchuana na klabu mbali mbali za mkoa huu kwa ajili ya mashindano maalum yaliyopangwa kufanyika Juni mwaka huu.


"Hali ya maandalizi yanakwenda vyema na inatoa dira ya kikosi kuchuana vikali na klabu zitakazojitokeza kushiriki mashindano hayo maalum kwa ajili ya kuinoa timu hiyo  tayari wakati wa mashindano ya taifa yanayokuja"alisema Nkungu.

Alisema wanariadha hao wanatakiwa kufanya mazoezi kwa bidii ili kuhakuikisha wanafanya vizuri zaidi katika mashindano hayo na anaimani watafanya vizuri.

"Nakiamini kikosi changu hivyo wanariadha wanatakiwa kujituma ili wafanye zaidi, hata hivyo nawaamini sana kwani ni wazoefu,"alisema

No comments:

Post a Comment