01 June 2012

TBL yatangaza tarehe ya kukabidhi zawadi


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager, jana imetangaza tarehe na zawadi zitakazokabidhiwa kwa wajasiriamali  ambazo ni vitendea kazi kwa walioshinda katika amshindano ya 'Wezeshwa na Safari Lager'.

Wajasiriamali hao watakabidhiwa zawadi katika matasha mbalimbali, ambayo yataandaliwa na kampuni hiyo.


Akizungumza Dar es Salaam jana Dar es Salaam Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema wajasiriamali hao watakabidhiwa ruzuku zao kwenye kanda walizofanyia mafunzo ya ujasiriamali.

“Tutaandaa matamasha ya kuwazawadia wajasiriamali wetu, ambapo tunawaalika pia wafanyabiashara wengine wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali wetu.

“Kituo cha Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi (kesho) katika Uwanja cha CCM Ilomba, Arusha litafanyika Juni 9 katika viwanja vya Soweto, Mwanza litafanyika Juni 16 katika Uwanja cha Furahisha na tutamalizia Dar es Salaam ambapo tamasha litafanyika Juni 23 kwenye viwanja vya Leaders Club,” alisema.

Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hao, Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa mashindano haya mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa.

Alisema fomu hizo zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili.

Shelukindo alisema wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndiyo waliopatiwa mafunzo.

Meneja huyo alisema wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na upungufu mbalimbali, kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara si za kwao na kutokuwa na biashara inayoendelea.

"Wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti kama mafundi wa kushona nguo za aina tofauti, mafundi seremala na magari.

"Wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku na kutengeneza mizinga ya nyuki, wengine ni wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua na teknolojia ya mawasiliano,” alisema.



Bwana Shelukindo aliwataja tena wajasiriamali watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.

Bwana Shelukindo aliendelea kuwataja wajasiriamali watakaojipatia ruzuku katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa.



Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano la Wezeshwa na Safari Lager, alisema “Shukrani nyingi ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwakaribisha kuhudhuria matamasha haya na aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na Safari Lager baadae mwaka huu.

No comments:

Post a Comment