13 June 2012
Mwanamke auawa katika fumanizi
Na Faida Muyomba, Geita
MKAZI wa Kijiji cha Mwagimagi, Wilaya ya Geita, mkoani Geita, Bi. Dome Shaban (35), ameuawa kwa kupigwa na mumewe baada ya kumfumania akifanya mapenzi na mwanaume mwingine.
Akizungumza na waandishi wa habati, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paulo, alisema tukio hilo lilitokea Juni 11 mwaka huu, saa nane usiku na kumtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Bw. Faida Anthony (45), ambaye ni mume wa mwanamke huyo.
Alisema mwanamke huyo alifumaniwa akiwa na mwanaume mwingine ambaye jina lake halikufahamika wakifanya mapenzi chumbani wakati mumewe hayupo.
“Mtuhumiwa aliporudi nyumbani aligonga mlango na kukuta mkewe akifanya mapenzi na mwanaume mwingine ambaye alifanikiwa kukimbia na hadi sasa hajulikani jina lake na mahali anapoishi,” alisema Kamanda Paulo.
Aliongeza kuwa, mtuhumiwa alichukua kitu chenye ncha kali na kumchoma sehemu ya jicho la kulia la kushoto kabla ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili hadi kusababisha kifo chake.
Alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya mauaji hayo ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Hiyo ni 'manslaughter'. Ni kosa la jinai. Si sawasawa kuua, na inabidi sheria ichukue mkondo wake akikamatwa.
ReplyDeleteHata hivyo ni jambo la busara kushauri wanandoa wajitahidi kuwa waaminifu katika ndoa zao. Kama kuna mashauri ya kuzungumzwa basi yafikishwe sehemu husika yazungumzwe na muafaka ufikiwe. Lakini kufanya uzinzi ni kosa kubwa maana inakuwa unabatilisha ndoa yako na pia kujiweka katika mazingira hatarishi kutokana na hasira kali za wivu wa mapenzi.
na mwanaume angekutwa anazini,mkewe angeweza kuua au ni mwanamke tu huuawa?
ReplyDeleteMara nyingi huwa wanaume tu ndo wanajifanya wanawivu zaidi mbona wawo wanaoa wake wawili na wala hawafanywi chochote lakini mwanamke jaribu kuwa na mabwana wawili utakiona cha moto
DeleteMara nyingi huwa wanaume tu ndo wanajifanya wanawivu zaidi mbona wawo wanaoa wake wawili na wala hawafanywi chochote lakini mwanamke jaribu kuwa na mabwana wawili utakiona cha moto
DeleteYesu alionya mwanamke tu kwamba, ondika na usirudie tena dhambi hii ndiyo maana wanaume wakienda nje ya ndoa hata kila saa, hawaonekani. Hivyo wanawake tunapaswa kujichunga sana maana ile laanailishika. Sasa tafakari wale wanaume walivyokuwa wengi na maamuzi yaliyotoka then uchuke hatua
ReplyDeletehuyo mwanaume achukuliwe ha2a kwani ingekuwa ni yeye kafumaniwa angeomba wayazungumze yaishe ila kwa vile ni mwanamke ameamua kuchukua hatua, istoshe na yeye atakuwa ana mwanamke mwingine, ndo maana anakuwa na wivu wa kijinga, angetakiwa kupeleka malalamiko sehemu husika na siyo kuchukua hatua ya kuua huyo anahitaji kunyongwa kama si kufungwa kifungo cha maisha.
ReplyDeletelakini kwa nini wanawake watoke mje ya ndoa, wanaume wengine they are too boring katika mapenzi...wanawake wanataka kupendwa na kubembelezwa...jifunzeni mapenzi. hata hivyo mama kama yamekushinda katika ndoa hiyo bora dai talaka lakini hakikisha chungu kimoja mwiko mmoja at a time..
ReplyDeleteDaaa!!!!!!!! Hii haivumiliki hata kama ni mke wangu wangu siwezi kutenda unyama huo. Mtuhumiwa anyongwe hadharani!!!!!! By Archi. S.F.Mang'ombe
ReplyDelete