07 June 2012
Kigogo CUF atimkia Chadema
Na Goodluck Hongo, Lindi
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimepata pigo baada ya Bw. Mohamed Madebe aliyekuwa meneja kampeni wa Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini, Bw. Salum Barwany, kukihama chama hicho na kukimbilia CHADEMA.
Uamuzi huo aliutangaza jana katika mkutano wa hadhara maarufu kwa jina la Okoa Mikoa ya Kusini uliofanyika Lindi Mjini.
Bw. Madebe alisema ameamua kukihama cha hicho kutokana na chama cha CUF kupoteza mwelekeo na kuyumbayumba.
"Nimeamua kukihama CUF kwa utashi wangu wenyewe bila ya kushurutishwa na mtu kwani hivi sasa chama hiki kimekuwa kikipoteza mwelekeo na kutokuwa na sifa kama awali, " alisema.
Aliwaomba wananchi wengine kumfuata, kwani CHADEMA inaoneka kuwa ni chama ambacho kimeonesha nia ya kubadilisha maisha ya umaskini kwa wananchi.
Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, alisema chama hicho kitaendelea na operesheni yake katika maeneo mbalimbali ili kuwaamsha wananchi waliolala na kunyanyukia CHADEMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Nimejaribu kuwatumia makala nyingi za afya na itafiti hazifiki, nifanyaje?
ReplyDeleteKINACHOPUNGUZA NGUVU ZA UPINZANI NI KUKOSA UMOJA KUKASHIFIANA WAO KWA WAO CHADEMA SI CHAMA CHA KITAIFA KAMA WANABISHA WAKAFANYE KAMPENI ZAO UNGUJA NA PEMBA NAWASHANGAA KUTENGANA NA CUF IKIZINGATIWA HAWAKUBALIKI VISIWANI SITAWASHANGAA WAKIHAMASISHA MUUNGANO UJADILIWE SI KWA LENGO LA KUUIMARISHA LA BALI NI KUUVUNJA ILI AZMA YAO YA KUONGOZA DOLA ITIMIE MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA TUKEMEE UNAFIKI NA SIASA ZA VURUGU NA UCHOCHEZI
ReplyDelete