10 May 2012
Wazawa watakiwa kuwekeza Tarime
Na Timothy Itembe
Tarime
MKUU wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara Bw.John Henjewele amewataka wazaliwa wa Tarime waliopo nje ya wilaya na nje ya nchi kuja kuwekeza Tarime kwa kuwa kuna amani na utulivu.
Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni kwenye kikao cha Mamlaka ya mji mdogo wa Tarime ikilichofanyika Halmashauri ya wilaya Tarime.
Bw.Henjewele alisema kuna asilimia kubwa ya watu amabo wanauwezo wa fedha na ni wazaliwa wa Tarime waliopo nje ya wilaya pamoja na nje ya nchi wakiwa na miradi mikubwa
ambapo sasa imefika wakati waje kuwekeza kwa lengo la kuendeleza Halmashauri
yao sanjari na wenyeji.
Aidha alibaini kuwa Mamalaka ya Mji wa Tarime inapanda kuwa Halmashauri
ya mji kwa hali hiyo inatakiwa vitege uchumi vya kuvutia watalii hali itayosaidia
mji huo kujipatia mapato mengi ya kijiendesha.
Pia Henjewele alikemea ujenzi holela unaojengwa na kuendeshwa na watu wachache
ambapo alisema kuwa kila anaye taka kujenga lazima apewe ramani na watu wa mipango
miji.
Kwenye kikao hicho mwenyekiti wa Mamlaka Bw.Christoph Mwita Mantago alitumia nafasi
hoyo kukemea baadhi ya wataalamu kutoheshimu maamuzi ya vikao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment