17 May 2012

'Wakuu wa Wilaya simamieni mfumuko wa bei Dar'


Na Heri Shaaban
Dar es Salaam

WAKUU wa Wilaya za Dar es Salaam wameagizwa kusimamie mfumuko wa bei ya vyakula katika masoko ya wilaya zao.

Agizo hilo limotolewa na Mkuu wa mkoa huo Bw.Meck Sadik mara baada kuwapisha wakuu wa wilaya zake.


Bw.Sadik alisema  kuwa kutokana na mfumuko wa bei katika bidhaa,anawagiza kutoa kipaumbe  kushughulikia suala hilo kwa kufanya  ziara katika masoko na kuangalia  bei ya vyakula.


Alisema kuwa katika masoko ya mkoa huo bei ya unga sembe kilo moja inauzwa shilingi 1200 hadi 1400 jambo ambalo wananchi wengi wanashindwa kumudu ukali wa gharama za maisha  na kulazimika kula mlo mmoja kwa siku.

"Serikali  imeshasambaza mahindi mengi kutoka katika  Ghala la Serikali  kwa kuwapa wafanyabiashara wakubwa kama Bakhresa  hivyo kwa sasa unga wa sembe utauzwa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo,"alisema Bw. Sadik.

Aliwataka wakuu wa wilaya hizo wawe na utaratibu ya kutembelea  masoko na kuangalia bei za bidha zinazopanda mara kwa mara.

Alisema  wafanyabiashara wote watakaouza unga sembe kwa bei kubwa badala ya bei ya serikali watachukuliwa hatua huku leseni zao zikikamatwa.

No comments:

Post a Comment