Na John Gagarini,
Bagamoyo
HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani imeadhimia kutoa kipaumbele
kwa miradi iliyobaki katika bajeti ijayo baada ya kuibuliwa hoja na
madiwani inayohusu miradi hiyo kutopewa kipaumbe katika bajeti
iliyopitishwa 2012/2013.
Diwani wa Kata ya Yombo Bw.Idd Mazongela alisema kwa kuzingatia umuhimu wa
kukamilisha miradi iliyobaki itajenga imani kwa wananchi ambao kwa kiasi
kikubwa huondoa imani kwa viongozi na serikali kwa kutokamilisha miradi hiyo .
"Wanaikataa miradi ya zamani lakini haina budi mtazamo ukaanzia kwa miradi
iliyodumu miaka kadhaa bila kumalizika ambayo mingine imeanza kuharibika
kabla ya utekelezaji," alisema Bw. Mazongera.
Madiwani wote waliunga mkono hoja hiyo na kudai ni zaidi ya miradi 100
katika sekta zote muhimu za afya, elimu na kilimo ambayo haijakamilishwa
wilayani humo.
"Wakuu wa idara kufanya kazi zao kwa kwenda sambamba na kutembelea na
kukagua miradi ili hali kuwezesha kupata ufahamu wa namna inavyoendelea na
hatimaye kupatiwa ufumbuzi," alisema Bw. Mazongera .
Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo imepitisha bajeti zaidi ya bilioni 33
huku ikitenga fedha kwenye elimu,afya na maji zaidi ya sh. bilioni 9.5
na kilimo sh. milioni 781,440,244
Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw. Samwel Salianga alisema katika
bajeti hiyo upande wa sekta ya elimu vyoo 15 ambavyo vilikuwa
havijakamilika kila kimoja kimetengewa zaidi ya sh. milioni moja
,vyumba vya madarasa 15 kila kimoja sh.milioni tano sawa na sh.milioni 75,na
nyumba za walimu wa shule za msingi mpya 28 kiasi cha sh. milioni 7 kwa
kila moja .
No comments:
Post a Comment