16 May 2012

Dkt.Nagu serikali imetoa kipaumbele maeneo ya uwekezaji


Na Tumaini Maduhu

WAZIRI wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt.Mary Nagu amesema kuwa Serikali imepiga hatua kwenye uwekezaji kwa kutoa kipaumbe kwa  maeneo yanayokuza ajira nchini kwa asilimia kubwa.

Akizungumza kwenye mkutano uliohusisha wadau kutoka sehemu mbalimbali za uwekezaji nchini Dkt. Nagu alisema kuwa Serikali imeamua kuyapa vipaumbele maeneo  hayo ili kupunguza tatizo la ajira nchini.


Alisema kuwa, faida nyingine yakutoa kipaumbele maeneo ya uwekezaji ,teknolojia mpya itaongezeka nchini pamoja na pato la Taifa kuongezeka.

"Sisi kama Serikali tumeamua kuyapa kipaumbele wawekelezaji wenye nia yakutokomeza tatizo la ajira nchini pamoja na  kuondoa utegemezi," alisema,Dkt. Nagu.

Katika hatua nyingine Dkt. Nagu alisema kuwa Tanzania imepiga hatua kwa kuuza bidhaa zao nchi za SADC ikiwa ni moja ya harakati zakuitambaulisha nchi yetu kwenye soko la biashara.

Kwa upande wake mshiriki kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi ya Tanzania (TPSF) Bi. Mary Kamathi alisema kuwa, mkutano huo umewajengea ujuzi na uzoefu katika kubadilishana mawazo juu uwekezaji hapa nchini.

"Tunaamini kupitia mkutano huu tutajifunza mambo mengi muhimu hususani hali ya uwekezaji inavyoweza kukuza soko la ajira nchini,"alisema,Bi. Kamathi.

No comments:

Post a Comment