15 May 2012
CHADEMA wasubiriwa Mkoani Mtwara
Na Godwin Msalichuma, Mtwara
WANANCHI mkoani Mtwara wamefurahishwa na ujio wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) utakaofanyika mapema siku za usoni kutembelea
jamii na kuzungumza nayo juu ya mambo mbalimbali.
Imeelezwa kubwa zaidi litakalozungumziwa ni mchakato wa Katiba Mpya ikiwemo Sensa ya Watu na Makazi.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi mkoani hapa walisema ujio huo una manufaa kwao.
Diwani wa Kata ya Kiromba Bw. Said Nahija alisema ni wajibu wao
kutembelea kwani watajifunza mambo kutoka katika jamii nayo itajifunza
kutoka kwao.
“Naona ni jambo jema kutembelea jamii na pia ni wajibu wao kwani kwa
kufanya hivyo unajifunza mambo mengi kutoka kwa jamii, lakini pia nayo
inajifunza kutoka kwenu hivyo binafsi nitafurahishwa kuona kuwa
wanafika na hasa vijijini kabisa,” alisema Bw. Nahija.
Bi. Happy Severin alisema anafurahi kusikia chama hicho wanafanya ziara ya kuja kutembelea wananchi kama waliyoifanya mikoa ya Kaskazini na kuahidi kuwa atakuwa wa kwanza kuchukua kadi na kuwa mwananchama kabisa.
“Nimesikia wanakuja huku kwetu CHADEMA hakika ninahaidi kuwa kama
watafika na kwenda vijijini kabisa nitakuwa mtu wa kwanza kujiunga na
wanipatie kadi yao niwe mwananchama kabisa…kwani tuliona na kusikia
walipofanya katika mikoa ya wenzetu sasa tunataka na sisi tushuhudie
huku kwetu,” alisema Bi. Severin.
Naye Ofisa Uhusiano wa chama hicho Bw. Tumaini Makene akizugngumza na gazeti hili kwa njia ya simu alisema, wana mpango wa kutembelea Mkoa wa Mtwara
kwa ajili ya kupata mitazamo yao katika mambo mbalimbali ukizingatia mwaka huu kuna matukio makubwa mawili, moja la kuchangia maoni ya Katiba Mpya na Sensa ya Watu na Makazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Bravo CDM,
ReplyDeleteHuu ndio uwajibikaji Hakuna kulala !!
Naomba kuwakumbusha wana CHADEMA wote nchini kuwa UHAI WA CHAMA UNATEGEMEA WANACHAMA HAI
ReplyDeleteKwa hiyo VIONGOZI wasisahau kuweka maudhuii mazuri ya kueleweka kuwa tunahitaji watu wawe hai katika kipindi chote cha wao kuwa wanachama. Kuwa na wanachama ambao hawalipii kadi zao ni kudhofisha chama. Lazima UKWELI HUU UFAHAMIKE.
Nawatakia kila la kheri. PEOPLES POWERRRRRRRR!!!