*Awashukia wanaotakiwa kujivua gamba
*Adai wanatumika kumuhusisha na ufisadi
*Asema ndani ya CCM wote si Richmond
*Adai wanatumika kumuhusisha na ufisadi
*Asema ndani ya CCM wote si Richmond
Katibu Mkuu wa CCM Bw.Wilson Mukama.
Agnes Mwaijega na David John
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Wilson Mukama, amedai kukerwa na baadhi ya watu wanaomuhusisha na ufisadi uliofanyika kwenye miradi ya machinjio, maji na kusisitiza yeye ni msafi.
Bw. Mukama aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya tuhuma dhidi yake ambazo zimetolewa katika vyombo vya habari vikimuhusisha na ubadhirifu wa fedha za miradi hiyo.
Alisema si kweli kwamba viongozi wote ndani ya CCM wanahusika na ubadhirifu katika miradi mbalimbali bali inawezekana tuhuma hizo zimeelekezwa kwake kwa sababu anahusika katika mapambano ya kuwavua magamba watu wanaokiuka maadili ndani ya CCM.
“Ndani ya CCM, si watendaji wote ni Richmond, inaonekana wengine wanatumia fursa hiyo kutaka kunichafua ili nionekane nashiriki ufisadi, mimi ni msafi nafanya kazi kwa kuzingatia maadili na nina wito ndiyo maana pamoja na kuwa mstaafu, bado nilionekana nafaa kuwa na wadhifa ndani chama,” alisema.
Aliongeza kuwa, taratibu za kisheria zipo hivyo kama kuna mtu ambaye mwenye hatia kwa tuhuma kama hizo kuna vyombo ambavyo vinaweza kushughulikia.
“Nashangazwa na baadhi ya watu kusema vitu ambavyo hawavijui undani wake, ni vema akaonesha uhalisia wa kitu anachokisema, miradi mingi ya maendeleo nchini inakufa kutokana na mabadiliko ya uongozi si ulaji wa fedha kama wengi wanavyodhani.
“Ieleweke wazi kuwa, miradi inakufa inapotokea yule aliyepewa nafasi ya kusimamia anapoondolewa na kuwekwa mwingine ambaye anashindwa kuuendeleza,” alisema Bw. Mukama.
Alisema kuna watu ambao hujitahidi kuonesha juhudi zao ili kuiwezesha nchi kupiga hatua lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuandamwa, kusakamwa na kusemwa vibaya bila wahusika kufanya uchunguzi yakinifu.
“Katika nchi hii wanaofikiri kwa kina na kuumiza vichwa kwa ajili ya mafanikio wanaandamwa kila kukicha lakini waliokaa tu, wanaachwa na kuonekana wa maana.
“Tatizo kubwa la nchi hii wajinga ni wengi kuliko waelevu lakini haiwezekani nchi ikawa chini ya uongozi wa wajinga na wahuni ambao hawawezi kuliletea taifa manufaa.
“Watu wanaleta siasa magazetini badala ya kujikita katika kazi za msingi lakini mimi najua ninachokifanya, siwezi kuendelea kuona nchi haina mabadiliko,” alisistiza Bw. Mukama.
Aliongeza kuwa, suala la kujivua gamba katika chama litaendelea kwa wananchama wote ambao wataonekana kwenda kinyume na maadili na taratibu za chama.
Akizungumzia utendaji wa kamati za bunge, Bw. Mukama alisema kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni masuala yanayojadiliwa katika kamati hizo hayakupaswa kuwafikia wananchi kabla ya kumfikia spika na kujadiliwa bungeni.
Alisema kazi ya kamati mbalimbali si kutoa taarifa zilizojadiliwa na wabunge kwenye kamati husika bali zipo kwa kurahisisha utendaji wa wabunge.
“Mimi sioni kama ni sahihi masuala ya kamati mbalimbali za bunge kujulikana kabla ya kufika bungeni ambako ndiko yanapaswa kutolewa maamuzi,” alisema.
katika nchi yenye wajinga wengi ni wazi pia wapo viongozi wajinga wengi na kama hivyo ndivyo basi hata wajinga na werevu hawana uwezo wa kujipima kwa kuwa wote watafanana kwa kuwa wengi ni wajinga hivyo kunakuwa na mjinga-mjanja ndio hao tunawaita werevu.NAUNGA HOJA MKONO
ReplyDeleteTATIZO KUBWA LA CCM NI KULINDANA KATIKA KUFICHA UKWELI. KAZI ZA KAMATI ZA BUNGE SIO KUFUNIKA MAMBO. WABUNGE KAMA MHIMILI WA UTAWALA BORA LAZIMA WAKIONA MAMBO YANAENDA VIBAYA LAZIMA WAPIGE KELELE. KAMA UKIHISI MTU FULANI NI MWIZI PIGA KELELE ILI WAHUSIKA WAMSHUGHULIKIE HUYO MWIZI. KAMA SIO MWIZI ATAJITETEA. HAPA HAKUNA CHA VIKAO VYA SIRI. VIKAO HIVI NDIVYO VINAVYOKUZA UFISADI.
ReplyDeleteNDG. MUKAMA, NENDA MAHAKAMANI AU PELEKA SUALA LAKO KWA UMMA KAMA UMEONEWA.
MUKAMA ASITUMIE STAILI YA CCM YA KUFICHA MAFISADIKAMA HAO MARICHMOND. KELELE ZIPIGWE ILI HAO MARICHMONDI WAASHUGHULIKIWE NA WOTE WANAOHUSIKA NA SIO KUPELEKA SUALA KAMA HILO KWENYE KAMATI NDOGO YA NIDHAMU YENYE WATU WACHACHE. HUKU NI KUFUNIKA MAMBO.
KAMATI ZA BUNGE MACHACHARI TUNAWAPA HONGERA SANA. FANYENI KAZI KAMA MLIVYOTUMWA NA BUNGE AMBALO NI SAUTI YA WANANCHI. HATA KAMA BUNGE LILILOWATUMA AMBALO LINA WINGI WA WABUNGE WA CCM LIKISEMA HAMTENDI KAZI VIZURI, BASI RUDINI KWETU WANANCHI ILI HAWA WABUNGE WASHUGHULIKIWE NA WANANCHI WENYEWE KWA NJIA ZA KIDEMOKRASIA KWA KUTUMIA SILAHA YA KURA ZAO IFIKAPO WAKATI WAKE.
PELEKENI TAARIFA ZENU BUNGENI ILI WANANCHI TUJUE HAO WATUHUMIWA NA KUTOA DATA ZAO ZAIDI. SASA HIVI TUMEFUMBULIWA MACHO KUWA FEDHA ZIMEFUJWA AU ZIMEIBWA WILAYA FULANI NA SASA TUNAUWEZO WAKUFUATILIA. KAMA MNGEFICHA HATUNGEJUA KWA MFANO FEDHA ZIMETUMIKA VIBAYA HUKO MONDULI N.K. TUTAJUA NI KWA NINI TUMEKOSA MAJI,BARABARA N.K.
BWANA MUKAMA AELEWE WAZI KWENYE HAYO MASHIRIKA NA SERIKALI ZA MITAA KUNA MAKARANI NA WAHASIBU WENYE UCHUNGU NA HIZO MALI ZINAIBWA KWA HIYO WATATOA SIRI ZOTE ZA HILA ZOTE ZINAZOTUMIKA KUIBA MALI ZA UMMA. HUWA WANATUAMBIA MTAANI KUWA HUYU KATAFUNA HIVI, HUYU KAPELEKA MTOTO ULAYA KWA FEDHA YA WIZI N.K
WATANZANIA TUMECHOKA NA JINSI SERIKALI YA CCM INAVYOWALINDA WEZI. MARA WAWAPIGE TRANSFER, KESI ZIPELEKWE MAHAKAMANI NA KUCHUKUA MIAKA BILA KUISHA ILI LABDA WATU WASAHAU. AU KUENDELEA NA CHUNGUZI ZISIZOISHA. KUTISHANA N.K.
VIVA MH. ZITTO NA MH. MREMA. KAZENI BUTI MFUNGE MAGOLI YA VISIGINO. WANANCHI TUKO NYUMA YENU. WANANCHI NI WENGI KULIKO WABUNGE AU CHAMA CHA CCM. MAFISADI NI WACHACHE KULIKO WANANCHI WALIOWATUMA BUNGENI KULINDA MALI ZAO. WAKIWAGUSA SISI TU NA NYIE.
Unatakiwa Mkama uharikishe kuwavua magamba la sivyo wewe utavuliwa kwani nia yao ni kukufanya kuwa bize na majungu ili kuendelea kuvuna wanaowaunga mkono.
ReplyDeleteGamba litaondoa Gamba?
DeleteHuwezi kuwa kiongozi wa CCM ambayo iliwekwa madarakani na mafisadi usiwe fisadi.Mukama kama angekuwa msafi angekihama chama,lakini atakula wapi?.
ReplyDeleteHahami Mtu. Mafisadi yatakula polisi au korti la the Hague ICC. Wewe subiri tu utaona.
DeleteTanzania ina wajinga wengi zaidi kuliko wenye maarifa kwa sababu CCM imegeuza ujinga ni mtaji wa kisiasa. Hakimu anapotoa maamuzi ya kijinga ili kufurahisha watawala na CCM wanamsifia na kufurahia ujinga , hayo ndio matokeo.
ReplyDeleteMaendeleo ya Africa ni ndoto tu kama Ujinga wenyewe ndio unatawala.
haya watu wakisema ukweli inakua hoja kwamba wanachafuliwa,mbona viongozi wengine wanafanya kazi zao vizuri mpaka wanastafu hawana doa iweje wewe tu uonekane,mkubwa jipange
ReplyDelete