*Polisi kuimarisha ulinzi maeneo mengi
Na Waandishi Wetu, Arusha
MACHO na masikio ya wafuasi na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo yanaelekezwa jijini Arusha ambapo Mahakama Kanda ya Arusha, itatoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Arusha Mjini.
Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na wapiga kura watatu ni ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo Bw. Godbless Lema (CHADEMA), dhidi ya mpinzania wake, Dkt. Batlida Burian (CCM).
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na Majira, walisema hukumu hiyo itatikisa jiji hilo ambapo taarifa za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali, zinadai ulinzi katika maeneo mbalimbali utaimarishwa ili kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani.
Hukumu hiyo inatolewa katika kipindi ambacho wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakisherehekea matokeo ya kura yaliyompa ushindi mbunge mteule wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari, huku CCM ikiwa inatafakari ni wapi ilijikwaa hadi mgombea wake, Bw. Sioi Sumari akabwagwa chini.
Siku ya jana katika baadhi ya maeneo, gumzo kubwa lilikuwa hukumu hiyo ambapo baadhi ya watu walisikika wakisema hukumu itakayotolewa iwe ushindi wa Bw. Lema au kutenguliwa, utatikisa jiji hilo.
Jaji ambaye atatengua kitandawili hicho ni Gabriel Rwakibarila wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga baada ya upande wa walalamikiwa kumkataa Jaji Joyce Mujulizi ambaye awali alipangiwa kusikiliza kesi hiyo kwa madai ya kutokuwa na imani naye.
Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo, upande wa Bw. Lema uliwasilisha mashahidi wanne. Katika uchaguzi huo uliofanyika 2010, Bw. Lema aliibuka mshindi kwa kura 56,169, wakati mpinzani wake Dkt. Burian akipata 37,460.
Pongezi kwa makala, sio za uchochezi. Tutampataje huyo mhusika??????
ReplyDeleteMungu Yu NA Mhe. Godbless Lema.
ReplyDeleteHata kama Bw.Lema atashindwa bado CHADEMA itasonga mbele.
ReplyDeleteNi vizuri kuzingatia uadilifu kupitia kauli zetu nyakati za kampeni. Naipongeza mahakama na wliofungua kesi dhidi ya lema. Lakini kwa kuwa sheria ni msumeno! Nawahamasisha watanzania na asasi za kuiraia wajitokeze kuwafungulia mashtaka wale wote waliotoa matusi mazito wakati wa kampeni za Arumeru mashariki, hususan wale wa chama tawala.
ReplyDeleteHukumu ya lema iwe ime-set precedence, matusi ya Arumeu hayapaswi kunyamaziwa. Nayo yasonge mahakamani hata kama waliotukana ni wanachama wa CCM. Mimi ni Mwanachama wa chama cha mapinduzi
ReplyDelete