19 March 2012

Uhamiaji yawatia hatiani Waethiopia

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma imewatia mbaroni wahamiaji haramu watatu raia wa Ethiopia kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini humo mwishoni mwa wiki, Naibu Kamishna, Norha Massawe alisema raia hao wa Ethiopia walikamatwa kwenye kizuizi cha mabasi kilichopo Nala nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma na maofisa uhamiaji mkoani humo.
 Kamishna huyo alisema, tukio hilo limefanikiwa kutokana na taarifa za awali ambazo zilitolewa kuwa kuna basi la abiria mali ya Mohamed Trans kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam limebeba abiria watatu ambao si raia wa Tanzania.
 “Ni vizuri kutoa taarifa mapema pindi, wahamiaji haramu wanapoingia ili tuweze kuwatambua na kuwafanyia kazi, hatimaye kulimaliza kabisa suala hili la uhamiaji haramu nchini,” alisema. Aidha Naibu huyo alidai kwamba operesheni ya kuwasaka wahamiaji hao ilianza mara baada ya basi hilo kuwasili mjini humo majira ya saa 11 jioni na kufanikiwa kuwatia mbaroni.
Hata hivyo Kamishna huyo aliwataja wahamiaji hao kuwa ni, Bw.Girma Anito (22), Bw.Zynu Womebo (30) na Bw. Mabeju Chengula (27) ambao wote ni raia wa Ethiopia. Pia alifafanua kuwa watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria. Vijana waliojiajiri kwa kunoa visu kwa kutumia baiskeli wakiwa nje ya Soko Kuu la Kariakoo, wakisubiri wateja Dar es Salaam jana. Picha na Bahati Mohamed
“Ni vizuri kutoa taarifa mapema p i n d i , wa h ami a j i h a r amu wanapoingia ili tuweze kuwatambua na kuwafanyia kazi, hatimaye kulimaliza kabisa suala hili la uhamiaji haramu nchini,”
Massawe
UNOAJI
HABARI ZA MIKOANI
Jumatatu Machi 19, 2012

No comments:

Post a Comment