Ulaya
Na Victor Mkumbo
MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni bondia wa ngumi za kulipwa nchini, David Mrope 'Zolla' D na Mbwana Mohamed 'MB Dog', wanatarajia kuanza kufanya shoo katika nchi mbalimbali barani Ulaya, kuanzia Machi mwaka Huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Zolla D alisema wamepata mwaliko wa kufanya shoo 10 nchini Ujerumani, pamoja na nchi mbalimbali.
Alisema wanatarajia kuondoka nchini Februari 27, mwaka huu na shoo hizo zitaanza Machi 3 mwaka huu.
Msanii huyo alisema katika shoo hizo, anatatajia kuimba nyimbo zake mbalimbali zikiwemo mpya na za zaman.
Alizitaja nchi nyingine watakazokwenda kuwani Norway, Uholanzi, Sweden, Italia na Ufaransa ambapo shoo shoo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya TIZO International na watu wa Ujerumani.
“Tunatarajia kuondoka nchini Februari 27, mwaka huu kwa ajili ya kwenda Ulaya kufanya shoo katika nchi mbalimbali na taratibu zote zinaendelea vizuri, ikiwa ni pamoja na kukamilisha hati za kusafiria,” alisema Zolla D.
ends......
No comments:
Post a Comment