01 February 2012

Vodacom yazindua promosheni ya punguzo



Na Mwandishi wetu

KAMPUNI  ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua  promosheni ya  punguzo la gharama za simu kupiga na kutuma ujumbe mfupi wa maneno- SMS itakayowahusisha wateja wa kampuni hiyo ambao  watapiga simu kwa gharama ya robo shilingi kwa sekunde.

Promosheni hiyo ya siku saba iliyoanza  Jumatatu Januari 30, 2012 inahusu kupiga simu za ndani ya mtandao wa Vodacom yaani kupiga Vodacom kwenda Vodacom kati ya saa nne usiku na saa moja asubuhi kila siku kwa wateja wote wa malipo ya kabla.

Aidha sanjari na ofa hiyo kamambe Vodacom imetoa pia punguzo la gharama ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno hadi shilingi 25 kwa ujumbe wakati wote wa siku kwenda mtandao wowote wa simu ya mkononi nchini kwa kipindi cha siku saba nayo pia  kuanzia jana Jumatau.

Akitangaza promosheni hizo mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema ni imani yake kwamba katika kipindi chote cha siku saba cha promosheni hiyo wateja watafurahia kwa kufanikishiwa mawasiliano ya  biashara, familia, kazi na mengineyo kwa gharama nafuu zaidi.

“Wateja wa Vodacom wakati wote wanafurahia huduma bora, nzuri na zenye kukidhi mahitaji halisi, ni wazi kipindi hiki cha siku saba cha promosheni hii ya punguzo la gharama za upigaji wa simu na utumaji SMS kitawapatia wakati mwingine bora wa kufurahia kuwa wateja wa kampuni inayoongoza soko,”alisema Bw. Rene.

Promosoheni hii inakwenda sawa na azma ya Vodacom ya kutoa fursa ya Watanzania kuunganishwa kimawasiliano na kubadili maisha.

“Ni fursa nzuri kwa wateja wetu, tunawaomba waitumie ikiwa ya kiwango cha chini zaidi  katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi nchini na Vodacom itaendeleza utamaduni wa kuwa kinara wa kubuni na kuleta sokoni promosheni pamoja na huduma zenye thamani na mantiki halisi ya wateja wetu na jamii nzima nchini,” alisema

No comments:

Post a Comment