Na Heri Shaaban
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala,imefuta kilio cha muda mrefu cha wakazi wa Kata Kipawa kwa kuwajengea kituo cha afya kitakachotoa huduma za mama na mtoto MCH ndani ya kata hiyo na maeneo jirani.
Akisoma taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya uchaguzi ya CCM kuanzia Juni 2011 hadi Desemba 2011 Diwani wa Kata hiyo,Bi.Bonnah Kalua alisema kuwa wakati alipokuwa akigombea udiwani ndani ya kata hiyo wananchi wake walimuelezea kuwa kata hiyo aina kituo cha afya.
"Halmashauri yangu kwa kushirikiana na wadau tumefanikisha ujenzi wa kituo hicho baada kupata eneo la kujenga"alisema Bi.Kalua.
Alisema kuwa kata hiyo ina mitaa mitatu mbayo ni Mogo,Kalakata na Kipunguni na ina wakazi zaidi ya 97,000 kati yao wanaume 48100 na wanawake 48600,kutokana na sensa iliyopita.
Pia alisema kuwa kero zingine alizoweza kuzitatua ni ujenzi wa barabara,visima vya maji,kuunda vikundi vya kijamii,kuboresha katika sekta ya elimu na kuunda vikundi vya ulinzi shilikishi.
"Kazi hizi zote nimetekeleza kutokana na ushirikiano mzuri na viongozi mbalimbali wa Serikali za mitaa na wanachi kwa ujumla.
Aliongeza kuwa kuwa sasa hivi ameanzisha mpango mkakati wa kumaliza kero ya madawati kwa shule zilizopo kata hiyo ili kuondoa tatizo la watoto kukaa chini.
No comments:
Post a Comment