Na Mwali Ibrahim
KITUO cha redio cha Times FM 100.5, kimeandaa usiku maalum kwa ajili ya kuuenzi Utamaduni wa Kiafrika ambao utazinduliwa rasmi kesho katika ukumbi wa Swizz Pub, Tabata.
Times kwa kushirikiana na Africa Mass Media, wameamua kuanzisha usiku huo ili kuuenzi utamaduni wa mwafrika,ambapo watakuwa wakitoa zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa na Super Markert ya TSN kwa watu watakao vaa kiafrika.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa mchakato huo, Michael Saduka alisema, kesho ndio utakuwa uzinduzi rasmi ambapo utakuwa ukifanyika kila siku Ijumaa ili kuweza kuuenzi utamaduni huo.
"Tumeamua kwa nia thabiti ya kumuenzi mwafrika, hivyo tunategemea watu watakaokuja katika burudani hii watakuwa wakivalia mavazi halisi ya kiafrika,tutakuwa tukitoa zawadi kwa watu waliovalia mavazi hayo," alisema Saduka.
Aliongeza kuwa sambamba na hilo, pia watakuwa wakiendesha mchakato wa kuibua vipaji kwa wasanii wachanga, ambapo kila Ijumaa watakuwa wakipanda wasanii tofauti tofauti na burudani itakuwa ikitolewa na Dj Mick love 'Saduka' na Dj R guy.
No comments:
Post a Comment