03 February 2012
Bilal awakemea wanaokosoa CCM
Na Salim Nyomolelo, aliyekuwa Pwani
MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dkt.Gharib Mohammed Bilal amesema watu wanaoendelea kukipaka matope Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nia ya kukichafua yatawageukia wenyewe.
Hayo aliyasema jana mjini Utete katika Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati akizungumza na wanachama wa CCM baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo.
Alisema, CCM ni chama ambacho kinategemewa katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kudumisha amani na upendo.
Hata hivyo, Dkt.Bilal alisema, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu kuanzia ngazi ya shina utasaidia katika kukipa uhai chama hicho.
"Baada ya uchaguzi huo tuatapata viongozi bora ambao watakuwa ni watendaji wazuri wa CCM katika kuongeza uhai wa chama chetu," alisema
Akizungumzia suala la matatizo yanayoendelea katika nchi, Dkt.Bilal alisema, hakuna nchi isiyokuwa na matatizo na kuongeza kuwa zipo nchi mbalimbali ambazo
zina matatizo.
"Matatizo yanayoendelea hapa nchini yapo kila mahali, kama uchumi na huduma za jamii nchi nyingi zimeshuka, ambapo jambo la msingi ni namna ya kutatua kwa kuwa uwezo upo na hivyo tusione tabu kuwa na matatizo," alisema
Alisema,nchi ina utajiri mkubwa wa watu na maliasili ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuwasaidia wananchi kuishi katia maisha bora.
Akizungumzia mchakato wa Katiba Mpya, Dkt.Bilal aliwataka wanachama hao kufuata taratibu na kutoa ushirikiano pindi zoezi hilo litakapoanza.
"Wakija viongozi wengine, wasikilizeni na mkiwa na maswali ulizeni, lakini mwisho wa siku nyie ndio mtakaofanya uamuzi," alisema Dkt.Bilal
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Pwani, Bi.Mwantumu Mahiza aliwaambia wanachama hao kuwa CCM ndio kila kitu huku wengine wakifuata nyuma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment