01 February 2012

Rais Jakaya Kikwete kuhudhuria kongamano

Na Amina Athumani

BARAZA la michezo Taifa (BMT) limesema linategemea Rais Jakaya Kikwete kuhudhuria kongamano kubwa la wadau wa michezo litakalozungumzia matatizo mbalimbali ya michezo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BMT, Henry Lihaya alisema juzi baraza hilo lilikaa kikao na kamati ya maandalizi ya kongamano hilo na wakatoa mawazo yao juu ya kongamano hilo.

Alisema watakaa tena kikao Februari 15 mwaka huu huku Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa mgeni rasmi katika kikao hicho.

"Bado hatujapanga tarehe rasmi ya kongamano hilo lakini kuna vikao vya kamati ambavyo jana tulikaa (juzi) na wadau ambao ni viongozi wa vyama vya michezo walitoa mawazo yao,"alisema Lihaya na kuongeza kuwa.

"Tutakua na kikao kingine Februari15 ambacho tunategemea Waziri atakuwepo nafikiri hicho ndicho kitatao tarehe ya ngomamano hilo ambalo tunategemea Rais Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi,"alisema Lihaya.

Kongamano hilo la michezo limekuwa likipigwa kalenda mara kwa mara na lilikuwa lifanyike tangu kipindi cha uongozi wa BMT uliokuwa chini ya Mwenyekiti wake Idi Kipingu.

Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Dioniz Malinzi pamoja na wajumbe wake wameadhimia mwaka huu kulifanya kongamano hilo ambapo tayari kamati ya maandalizi imeanza vikao vya pamoja kwa ajili ya kongamano hilo.


No comments:

Post a Comment