Na Edmund Mihale
BARAZA la Mitihani (NECTA) limetangaza matokeo ya Mitihani ya Maarifa (QT) na Kidato cha Nne (CSEE) uliofanyika Oktoba mwaka jana huku kukiwa na ongezeko kubwa zaidi la udanganyifu kuliko mwaka jana.
Katika matokeo hayo watahiniwa 3,303 walibainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo kati yao 3,301 ni wa CSEE na wawili ni wa marifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Mkuu ya Baraza hilo, Dar es Salam jana, Katibu Mtendaji NECTA, Dkt. Joyce Ndalichako alisema kuwa watahiniwa 2,896 walibainika kuwa na mfanano wa majibu usio wa kawaida.
Alisema kuwa wengine 182 walibainika baada kukamatwa na wasimamizi wa mtihani ndani ya wakiwa na majibu, notisi, simu selula, kusajiliwa mara mbili, kufanya mtihani kwa kutumia karatasi za majibu zenye miandiko tofauti katika somo moja.
Alisema udanganyifu mwingine ni kubadilishana karatasi za maswali, karatasi za kujibia mitihani ili kuandikia majibu au kujadiliana ndani ya chumba cha mtihani ,kufanyiwa mtihani na watu wengine, kukamatwa na zaidi ya moja ambazo hakupewa na masimamizi wa mtihani.
Alisema kuwa watahiniwa wengine walibainika kuwa na kesi mbili tofauti kama mfanano wa majibu, notesi za masomo, karatasi za kujibia mtihani zaidi ya moja, kubadilisha karatasi ya majibu .
Mbali na hayo, Dkt. Ndalichako alisema kuwa, baraza hilo pia limewafutia mitihani watahiniwa wanane walioandika matusi katika karatasi za majibu kitendo ambacho ni kosa la utovu nidhamu katika mtihani kwa mujibu wa kifungu cha 5 (13) cha kanuni ya mitihani.
"Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi ya majibu kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu na Baraza la Mitihani Tanzania halitaweza kuvumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo hivyo pamoja na kuwafutia matokeo ufautialiaji zaidi utafanyika ili kuona hatua zaidi wanaweza kuchukuliwa tayari tumepeleka vilelezo polisi kwa hatua zaidi'',alisema.
"Napenda kuwaasa watahiniwa wa kidato cha sita walioanza mtihani wao wa kidato cha sita leo (jana) kujiepusha na udanganyifu huo katika mitihani na pia kuepusha mitindo wa kuandika matusi katika karatasi za majibu au mambo yasiyohusiana na mitihani" aliasema Dkt Ndaliachako .
Alisema pia wapo walioacha kujibu maswali walioulizwa katika mtihani huo na kuandika nyimbo za bongo fleva, rap na kuchora picha za wachezaji mpira katika karatasi za kujibu mtihani.
Alisema kuwa wapo waliokamatwa wakiwa na majibu katika rula , viungo vyao vya mwili sehemu mbalimbali kama katika mapaja, viganjani, vitambulisho madaftari makubwa (Counter book) na pindo za nguo.
Alisema kuwa mmoja kati yao alikamatwa akiwa ameandika majibu ya mtihani katika mkono wa shati lake hivyo msimamizi wa mtihani huo alikata kipande cha mkono na kuweka kama ushahidi.
"Hapa mnaona ni kipande hiki cha nguo kilikatwa na msimamizi baada ya kubaini kuwa huyu jamaa alikuwa na majibu katika shati lake hivyo alikikata na kuambatanisha na karatasi yake ya majibu kama ushahidi na kuuleta kwetu tunampongeza kweli msimamizi huyu," alisema Dkt Ndalichako.
Hali halisi ya matokeo
Dkt. Ndalichako alisema kuwa watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 waliofaulu mtihani huo mwaka jana wasichana ni 90, 885 sawa na asilimia 48 .25 ya wasichana waliofanya mtihani na wavulana 134,241 sawa na asilimia 57.51 ya wavulana waliofanya mtihani ukilinganisha na watahiniwa 223,085 sawa na asilimia 50.74 ,
Watahiniwa katika shule
Alisema kuwa watahiniwa wa shule 180,216 sawa na asilimia 53.59 ya waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wamefaulu , wasichana waliofaulu ni 69,913 sawa na asilimia 44.36 na wavulana ni 110,303 sawa na asilimia 53.53 wakati mwaka jana watahiniwa waliofaulu walikuwa 177,021 sawa na asilimia 50.40 ya watuhumia waliofanya matihani huo.
Watahiniwa wa kijitegemea
Watahiniwa kujitegemea waliofaulu mtihani huo ni 44,910 sawa na asilimia 52.52 ya waliofanya mtihani huo wasichana waliofaulu ni 20,972 sawa na asilimia 47.90 na wavulana ni 23,938 sawa na asilimia 57. 38 wakati mwaka 2010 watahiniwa wa kujitegemea 46,064 sawa na asilimia 52.09 ya waliofaulu.
Ubora wa ufaulu
Alisema ubora wa ufaulu kwa kungaliwa madaraja lisema kuwa wataihiniwa wa shule unaonesha kuwa wataihiniwa 33,577 sawa na asilimia 9.98 wameafaulu katika madaraja kwanza hadi la tatu wasishana waliofaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ni 10, 313 sawa na asilimia 7.13 na wavulana ni 23, 264 sawa na asilimia 12.13
Shule kumi bora katika kundi la watahiniwa zaidi ya 40
Dkt Ndalichako alizitaja shule hizo kuwa ni na idadi ya wanafunzi katika mabano kuwa ni St. Francis Girls ya Mbeya (86), Feza Boys SS YA Dare sa Slaam (56), St Joseph Millenium ya Dar es Salaam (115), Marian Girls ya Pwani (114), Don Bosco Seminary, Iringa (45), Kasita Seminary, Morogoro (42), St Marys Mazinde Juu, Tanga( 79), Canossa Dar es Salaam (61), Mzumbe Morogoro (111) na Kibaha SS, Pwani ( 105) .
Kumi za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 40
Alizitaja shule hizo kuwa ni Bwebwera ,Tanga (48), Pande Daraja Tanga (77), Mafundia , Tanga (91), Zirai Tanga (53), Kasokola Rukwa (42) Togoni, Tanga (64) Mofu, Morogoro (59), Mziha, Morogoro (43) Maneromango Pwani (110) na Kabuta, Pwani (91).
Shule kumi bora zenye watahiniwa chini ya 40
Alizitaja kuwa ni Thomas More Machira Dar es Salam (25) Feza Boys Dar es Salam (36), Dungunyi Seminary Singida (28), Maua Seminary Kilimanjaro (32) St Josefu Kilocha Iringa (36), Sengrema Seminary, Mwanza (34), Lumumba Unguja (32), Quuen of Apostels Ushirombo Shinyanga (24), Bihahawana Junior Seminary Dodoma (37).
Shule 10 za mwisho zenye watahiniwa chini ya 40
Dkt Ndalichako alizitaja shule hizo kuwa Ndongosi, Ruvuma (4), St. Luke Ruvuma (6), Igigwa, Tabora (11), Kininginila Tabora (15) Ndaoya Tanga(15), Kilangali Morogoro (28), Kikulyungu Lindi (16), Usunga, Tabora (26), Mto Bubu Day Dodoma (37), Miguruwe Lindi (13),
Wanafunzi 10 bora kitaifa
Aliwataja kuwa ni Moses Swai kutoka Fedha Boys Dar es Salaam, Rosalyna Tandau, ( Marian Girls Dar es Salaam), Mboni Maumba St Francis Girls Mbeya),
Sepiso Mwemelo (St. Francis Girls Mbeya ), Uwela Rubuga (Marian Girls Pwani), Hellen Mpanduji (St. Marys Mazinde Juu Tanga) Daniel Wallance Maugo, (St. Joseph Millenium Dar es Salaam), Benjamini Tilubuzya (Thomas More Machira Dar es Salaam ), Simoni Wiliam Mbangalukela (St. Joseph Millenium Dar es Salaam) na Nimrod Tutatora (Feza Boys Dar es Salaam )
wanafunzi wengi hufeli kwa sababu ya vitendea kazi (sehemu za kukaa, vitabu husika vya kusoma na kufundishiwa, maabara,mazingira ya kusomea i.e kifikra na n.k,ukosefu wa mbinu za kufundisha kwa waalimu,majukumu kwa wanafunzi wa kutwa, n.k),hivyo yatupasa wazazi pamoja na serikali tuwajengee wanafunzi mazingira ya kufurahia shule kama wale wanaosoma shule binasfi. Na Michael Z Costantine, FOCDTANZANIA- ARUSHA
ReplyDelete