16 February 2012

Kesi ya ulanguzi ya muandama Rais Zuma

JOHANNESBURG,A.Kusini

CHAMA cha Democratic Alliance cha nchini Afrika Kusini  kinasema kuwa uamuzi wa mwendesha mashataka uamuzi wa kuondoa mashataka dhidi ya Rais Jacob Zuma ulichukuliwa kwa misingi ya kisiasa na sio kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na chama hicho, katika kipindi hicho chama cha ANC kilishuhudia mvutano mkali wa kisiasa na kulikuwa na madai kuwa idara za serikali zilikuwa zinatumiwa kuwanyamazisha mahasimu wa kisiasa waliokuwa wanang'ang'ania madaraka.


Katika kipindi hicho mkuu wa kitengo maalum cha upelelezi cha polisi maarufu kama scorpions na mwendesha mashtaka walidaiwa kufanya njama ya kummaliza kisiasa Rais Zuma.

Kanda za mazunguzmo hayo kati yao zilitumika mahakamani kama ushahidi wa njama hiyo.

Mwaka wa 2007, Jacob Zuma alifunguliwa mashataka ya kuhusika na rushwa, udanganyifu na ulanguzi.

Kesi hiyo dhidi yake iliwasilishwa siku nane baada ya kumshinda aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Bw.Thabo Mbeki kwenye mvutano wa kukiongoza chama cha ANC.

Mashtaka hayo yaliibuka baada ya aliyekuwa mshauri wa masuala ya kiuchumi wa Rais Zuma,Bw. Shabir Shaik alipopatikana na hatia ya ulanguzi.

Mashtaka dhidi ya Rais  Zuma yaliondolewa, wiki mbili kabla uchaguzi wa April mwaka 2009 hatua ambayo  iliwaudhi viongozi wa upinzani na baadhi ya mashirika ya kijamii nchini humo.

Wakosoaji wanasema lazima mahakama iamue ikiwa kweli kiongozi huyo alikuwa na hatia na  uamuzi wa mahakama kuu kuhusu kesi hiyo unasubiriwa kwa hamu.


No comments:

Post a Comment