06 February 2012

Kalunde kukamilisha albamu karibuni

BENDI ya muziki wa dansi ya Kalunde, ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha albamu yake ya pili ambayo inatarajia kutoka hivi karibuni.

Akizungumza Dar es Salaam jana kiongozi wa bendi hiyo, Bob Rudala alisema kwa asilimia kubwa albamu hiyo imekamilika isipokuwa nyimbo moja bado haijakamilika.

Alisema kwamba wamechukua muda mrefu kutengeneza albamu hiyo, ili waifanye kwa ubora wa hali ya juu na kuwa tishio kwa bendi nyingine.

Rudala alizitaja nyimbo ambazo zimekamilika na baadhi yake kupigwa katika kumbi mbalimbali za dansi kuwa ni Mama yangu, Sisee na Imebaki stori.

Alizitaja nyimbo nyingine kuwa ni Fungua, Ulinipendea nini, Nilie na nani pamoja na Njoo tucheze ambao upo katika hatua za mwisho kukamilika.

"Imetuchukua muda mrefu kukamilisha albamu hii ya pili kutokana na kwamba tunataka kutengeneza kitu chenye ubora wa hali ya juu, ili wateja wetu wafurahie," alisema.

Bendi hiyo mwaka juzi ilizindua albamu yake ya kwanza ya Hilda, ambayo nyimbo zake zinatamba katika vituo mbalimbali vya redio.

Albamu hiyo ina nyimbo za Hilda, Itumbangwewe, Nataka kuzaa na wewe, Kiliokilio, Fikiria na Maiwane.

No comments:

Post a Comment