22 February 2012

Kahawa yapewa kipaumbele Tarime

KAHAWA inaingizia Halmashauri ya Tarime zaidi ya sh.milioni 96 kuanzia Desemba 2011 hadi Februari 2012 ikiwa ni makusanyo ya ndani.
 

Halmashauri hiyo imepanga ikusanye   ushuru wa  zaidi ya sh. milioni 100 kutokana na zao la kahawa ikiwa ni mapato ya ndani kwa ajili ya kukuza uchumi wa Halmashauri ya Tarime.

Hayo yalibainika kwenye kikao cha wadau wa mchakato wa kuandaa mpango wa maendeleo ya kilimo ya wilaya kilicho fanyika jana.

Akitoa maelekezo kwenye washa hiyo ya siku moja kwa ajili ya kupendekeza zao maarufu wilayani hapo, Ofisa Kilimo Uvuvi na Mifugo wa wilaya Bw.Slyvanus Gwiboha alisema kuwa
tiyari  kahawa limeipatia halmashauri zaidi ya sh. milioni 96 kwa kipindi cha  miezi 3 na serikali imetoa ruzuku ya sh.milioni 25 katika halmashauri hiyo.

Katika kikao hicho kahawa  ilipendekezwa kuwa zao maarufu katika Wilaya ya Tarime ambapo litapewa kipaumbele katika mpango wa Mkukuta.

Wadau walichangia maoni mbalimbai ya kupendekeza  zao maarufu la wilaya ambapo katika washa hiyo Mbunge wazamani Bw.Charles Mwera alitoa hoja kuwa kuna haja ya kuwa na mazao
mawili ya wilaya ambapo pia alichukua nafasi hiyo kupendekeza kuwa moja litakuwa zao la kahawa sanjari na Zao la Mifugo Ng'ombe na kuungwa mkono wa wajumbe wengine.




No comments:

Post a Comment