02 February 2012

JNY Unit yakamilisha tatu mpya

Na Victor Mkumbo

KUNDI jipya la muziki wa kizazi kipya nchini JNY Unit, limekamilisha nyimbo tatu mpya ambazo zimeshaanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza Dar es Salaam jana, kiongozi wa kundi hilo, Deogratius Mongela 'King Desamo' alisema wameshakamilisha nyimbo tatu ambazo wamezirekodi katika studio ya Difatality Records.

Alizitaja nyimbo ambazo zimekamilika kuwa ni Ngoma ya Club, Mpweke na Carolite.

Alisema kundi hilo linaundwa na wasanii 11 kutoka katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambao wanaimba nyimbo za staili tofauti tofauti.

King Desamo alisema kwa sasa wapo mbioni kukamilisha nyimbo mbalimbali, ambazo zitakuwepo katika albamu hiyo ya kwanza itakayotoka mwishoni mwa mwaha huu.

Alisema pia wanatarajia kuanza kufanya maandalizi ya kurekodi video za nyimbo zilizokamilika, ili kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa muziki nchini.

“Tumeshakamilisha jumla ya nyimbo tatu, ambazo zimeshaanza kupigwa redioni na pia zinashika chati za juu, hivyo kwa sasa tunataka kukamilisha idadi ya nyimbo 15 ili tuweze kutoa albamu ya kundi, ambayo itatoka mwishoni mwa mwaka huu,” alisema

No comments:

Post a Comment